Header Ads Widget

IGP SIRRO ATAKA MMILIKI WA COSTA ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU 20 ASAKWE

 


MKUU wa jeshi la Polisi nchini (IGP) Saimon Sirro ameagiza mmiliki wa Costa iliyosababisha vifo vya watu 20 wilayani Mufindi mkoani Iringa kusakwa ili kuchukulia hatua za kisheria Kwa kuruhusu basi lake kufanya kazi ya kubeba abiria bila kuwa na Kitabu Cha Tiketi .Mwandishi wa Matukio DaimaAPP Francis Godwin anaripoti


"Hataruhusiwa kuchukua gari lake Polisi hadi atakapopatikana ili atueleze aliruhusu vipi gari lake kufanya kazi ya abiria bila kuwa na Kitabu Cha Tiketi"

Pamoja na Kutangaza kumsaka mmiliki huyo pia IGP Sirro amepiga marufuku magari yasiyo ya abiria kubeba abiria na kuwa msako mkali utafanyika ili kuchukua hatua Kali .

Akizungumza Leo mjini Iringa baada ya kuwatembelea Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa Katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ,Sirro alisema kuwa jeshi la Polisi limejipanga kuchukua hatua Kali Kwa madereva wasiofuata sheria na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi akiwa eneo la ajali 
Hata hivyo Sirro aliwataka watanzania kutokubali kupanda basi lolote ambalo halitoi tiketi Kwa Abiria wake .

Alisema sheria inawataka wenye vyombo vya Kusafirisha abiria kutoa tiketi Kwa wasafiri na kutofanya hivyo ni kosa kisheria .

Mganga mfawidhi wa Zamu wa Hospital ya Rufaa mkoa wa Iringa Jasmine Kachemela alisema Hadi Sasa Majeruhi wanne ndio wamepokelewa na wanaume wawili na wanawake wawili na kati yao mmoja yupo mahututi na maiti zipo 9 na 7 bado hazijatambuliwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI