Chama Cha Waandishi wa habari kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania Kwa kushirikiana na Open Knowledge foundation Leo imewanoa wanahabari juu ya uhifadhi na utunzaji wa fukwe Nchini
June 1 hadi Juni 11 ni siku maalumu ya maadhimisho ya siku ya uwazi wa takwimu Duniani
Maadhimisho hayo yamelenga kuwafundisha waandishi wa habari umuhimu wa takwimu kulinda fukwe zilizopo nchini na kuhakikisha zinahifadhiwa Ili kuendana na Hali iliyopo Kwa Sasa.
Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa OJADACT Edwin Soko ameeleza kuwa fukwe za Afrika Mashariki huchangia uchumi wa Nchi za Afrika Mashariki Kwa asilimia 57 kwa pato la Mwaka, hivyo Kuna umuhimu wa kuzitunza fukwe.
Aidha amewasihi waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhakikisha inaandika habari za fukwe zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na kufahamu takwimi mbalimbali za fukwe zilizopo nchini.
0 Comments