Diwani wa Kata ya Luhunga Adam Mgovano kulia akiwa ameshika bendera ya Taifa wakati wa kuliombea Taifa juzi.
...........
Diwani wa Kata ya Luhunga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Adam Mgovano ametoa Wito Kwa waumini wa dini mbali mbali kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na Taifa ili Maendeleo yazidi kuonekana na Amani izidi kutawala .
Diwani Mgovano ametoa Rai hiyo wakati wa ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika juzi Katika kanisa la Wasabato Igoda kata ya Luhunga Kwa kushirikiana madhehebu mbalibali yaliyopo kata ya Luhunga.
Amesema kazi ambayo Rais na Serikali imekuwa ikifanya ni kubwa na hivyo ili kazi hiyo izidi kuonekana ni lazima Kila mmoja kuendelea kuomba Kwa ajili ya Viongozi kuanzia ngazi ya vijiji ,wilaya na Taifa .
Awali mchungaji Sprian Mtweve akiongoza maombi hayo alitaka Kila mmoja kuendelea kuombea Taifa maana Amani inapotoweka madhara yake ni makubwa na hata kutolea mfano vita ya Ukreine na Urusi
0 Comments