NA HADIJA OMARY MATUKIO DAIMA APP LINDI
TAASISI ya Makumbusho ya taifa kitengo cha mali kale yameanza mchakato wa mpango wa kulitunza na kulihifadhi eneo la Tendeguru Wilayani Lindi Mkoani humo ambalo lilipatikana mabaki ya Mjusi Mkubwa Duniani aina ya Dainaso
Mpango huo umeanza kwa kuwakutanisha viongozi wa ngazi ya Vijiji na kata zilizopo katika eneo hilo katika warsha ya siku mbili ikiwa nalengo la kukusanya maoni juu ya uhifadhi na uendelezaji wa Eneo la Tendeguru ili liweze kuleta tija kwa Taifa.
Akizungumza katika Warsha hiyo Muhifadhi mwandamizi na Mtafiti kutoka Makumbusho ya Taifa DKT, Maximilian Chami alisema kuwa Mpango huo miongoni mwa michakato inayoendelea katika Taasisi hiyo katika kuliendeleza Eneo la Tendeguru ikiwa pamoja na kuliingiza kwenye maeneo yanayotambulika na UNESCO kuwa ni ya Urithi wa Dunia
Alisema ili Eneo liingizwe kwenye vivutio vya uridhi wa Dunia kunavigezo kumi ambapo kwa Eneo la Tendeguru linakidhi kigezo namba 7 ambacho ni Eneo ambalo linaelezea Maisha ya Viumbe au Historia ya viumbe ambavyo viliishi Dunia uniani na kupotea miaka mingi iliyopita .
Aidha Dkt. Chami alisema kuwa katika kuchagiza sifa hizo lazima kuwepo ama kuandaa mipango ya usimamizi katika eneo husika ambayo itaeleza mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya kusimamia na kuendeleza eneo hilo.
Alisema katika Warsha hiyo imehusisha kupanga mipango na mikakati mbali mbali ya kuifadhi na kuendeleza maeneo ya mali kale, kujadiliana na kushauriana namna bora ya kutekeleza mipango ya maendeleo ikiwa sambamba na kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika eneo hilo la Tendeguru
Awali akiungumza na wadau hao wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga aliwataka wadau hao kuendelea kulinda na kulihifadhi Eneo hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.
Ndemanga alisema Eneo hilo ni muhimu na lakipekee kwa Watu wa Lindi kwani Eneo hilo ni utambulisho kwa Mkoa huo hivyo linapaswa kulindwa , kutunzwa na kulihifadhi kwa faida ya sasa na Baadae
“Sisi sote ni mashahidi kuwa Eneo hilo la Tendeguru ni eneo maarufu siotu kwa Tanzania bali Duniani ni Eneo ambalo Dainaso walioishi miaka mingi sana Zaidi ya miaka milioni 150 mabaki yake yalionekana pale kwahiyo ni Eneo Maarufu sio tu kwa wana Lindi bali kwa Watanzania kwa ujumla”
Kwa upande wake Yazidu Mwenda Afisa Mtendaji wa Kata ya Kitomanga licha ya kuipongeza Taasisi hiyo kwa kuanzisha mpango huo ambao utaleta tija kwa wananchi wa Lindi na Nchi kwa ujumla akiiomba Taasisi hiyo kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi wa maeneo hayo kuendelea kulilinda na kuliifadhi Eneo la Tendeguru kwa Manufaa ya Taifa kupitia mikutano na Makongamano mbali mbali
0 Comments