Header Ads Widget

WAMAASAI MAKINI KWA KILA JAMBO II

 



Adeladius Makwega-DODOMA


Utani katika kabila la kimaasai unaonekaana pia katika hatua mbambali, kwanza kabisa katika koo za Kimaasai. Katika jambo hili kwanza msomaji wangu naomba uzitambua koo chache za kimaasai kama vile MOLLEL, LUKUMAI, LAISER na KIVUYO.


Koo zote hapo juu nilizozitaja zinatamkikia kimaasai kama ifuatavyo MOLLEL- ILOMOLLELIAN, LUKUMAI- ILUKUMAI, LAISER- ILAISER- na KIVUYO- ILHIVUYONI


Utani upo baina ya koo hizi lakini pia unapatikana kwa wanajamaa waliomo ndani ya koo yake. Kwa mfano tangu enzi ukoo wa MOLLEL unafahamika kama ni ukoo mkubwa, wenye jina kubwa huku wakiwa si matajiri. Japokuwa sasa wapo akina LAIZER walio matajiri lakini awali hawakuwa koo tajiri ya Kimaasai.


Asili ya jina LAIZER inatokana na kibuyu kikubwa cha kunyea maziwa, kunyea damu au kibuyu cha kunyea dawa hata hutumika kunyea kitu cha asili kinachoitwa MOTORI. 


Historia ya  kabila la Kimaasai inasema kuwa  ukoo wa Laizer ndiyo waliokuwa wakwanza kukitumia kibuyu hicho katika jamii hiyo.


Kibuyu hiki kwa Kimaasai kinafahamika kama OLAISERI na wale waliokileta kibuyu hicho katika jamii hii wakaitwa ILAISER naye baba wa ILAISER alifahamika kama LAISER.


Hata mzaliwa yoyote wa LAISER anapokwenda kuomba chochote kwa koo zingine za Kimaasai atasema nipe kwani wewe hautambua kuwa mimi ni LAISER. Hapo lazima atapatiwa kitu hicho alichokiomba bila ya shaka yoyote ile.


LUKUMAI huu ni ukoo ambao kwa asili walikuwa wakiutazama kama ukoo wa wanaojipenda wenyewe, huku wakiwa pia wachoyo. Inaaminika kuwa jina hilo lilitokana na tukio moja ambapo kulikuwa na sherehe na ndipo watu wazima wawili waliondoka na pande la nyama iliyokuwa inachomwa na kutokomea nayo kula wenyewe.


Jamaa hawa ndipo walipopewa jina la OLOIKUMAI likimaanisha kuwa jamaa huyo ni mchoyo na hataka kukaa na wenzake kula nao pamoja, kwa tafsiri ya kawaida OLOIKUMAI maana yake ni KOBE.


Hata sasa mtu anaweza kuomba kitu kwa Lukumai na naye Lukumai anaweza kumnyima kwa dhana ile ya maana ya jina la ukoo wake. Kulingana na mila za asili za Wamaasai kila ukoo wanamiliki ng’ombe zao na huwa na alama za kutambulika kwa rangi.


Mathalani MOLLEL ng’ombe zao huwa nyeusi naye LAIZER ng’ombe zao huwa nyeupe na pale ng’ombe inapopotea kutoka upande wa ukoo mmoja kwenda kwa mwingine utafutwa na ikikutwa na mwenye ng’ombe hiyo katika zizi anaondoka nayo na kama hakuna mwenyewe basi hubaki hapo.


Ukoo wa MOLLEL na KIVUYO huwa ni koo rafiki mno wakiwa na udugu wa tangu kwa mababu.Ukoo wa LAIZER, MOLLEL, KIVUYO na LUKUMAI kama pametokea ugomvi hapo awali na umesabaaisha shida yoyote walikuwa na desturi ya kukutana pamoja na kulijadili jambo hilo na kumlipisha faini mkosajin kinyume chake mkosaji na hata familia yake ilipewa adhabu.


Je kipi kitaendelea subiri matini ijayo


makwadeladius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI