Na Amon Mtega, Songea.
Daniel Kapinga mkazi wa Makambi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambaye ni hunywa bia moja ndani ya dakika moja au sekunde 50 bila kupumzika amelalamikia kushuka kiwango cha unywaji tofauti na awali .
Malalamiko hayo ameyatoa jana wakati alipoibuka mshindi wa unywaji wa bia chupa moja kwa kutumia dakika moja na sekunde moja kwenye mchezo wa bonaza wa kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii kufuatia kazi anazo zifanya kwenye jimbo hilo.
Kapinga akizungumzia unywaji wa bia huo kwenye bonaza hilo lililofanyika uwanja wa michezo wa shule ya msingi makambi iliyopo kata ya Ndilimalitembo alisema kuwa amesikitishwa kushuka kwa kiwango chake cha unywaji kutoka sekunde 50 hadi dakika moja jambo ambalo amesema siyo dalili nzuri kwake na kuwa atahakikisha anarudi kwenye kiwango chake cha ubora.
Mnywaji huyo ambaye walishindanishwa wanne kwa kunywa bia iitwayo bingwa amefafanua kuwa mara kadha amekuwa akiibuka mshindi kwa kuwaacha wenzake mbali lakini ushindi wa sasa unamtia wasiwasi kutokana wapinzani wake kumsogelea kwa dakika.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye bonaza hilo amempongeza kijana huyo kutoa burudani ya ushindani huo jambo ambalo limeibua furaha nyingine kwa washiriki wa bonaza hilo ambalo liliandaliwa na diwani wa kata ya Ndilimalitembo Issa Chiweneke kwaajili ya kuipongeza Serikali na Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro .
Katika bonaza hilo michezo mbalimbali ilichezwa ikiwemo mpira wa miguu,kufukuza kuku ,kukimbia na magunia kuonyesha vipaji vya uimbaji kutoka kwa wasanii mbalimbali chipukizi waliyopo kwenye Manispaa hiyo.
0 Comments