Header Ads Widget

DC MTWARA, TPDC WAHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI

 


Mwandishi wetu, Mtwara


 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya  amewahamasisha wanafunzi wa shule za Sino, Ndumbwe na Sabodo kusoma masomo ya sayansi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi katika sekta ya viwanda nchini.


Kauli hiyo ameitoa leo katika wakati wa  akitoa zawadi kwa washindi wa shindano la insha ya gesi asilia iliyoshindanisha shule 15 ambapo shule tatu ndio zilitoa washindi na kukukabidhiwa kitita cha shilingi 450,000 .


Katika shindano hilo mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha shilingi laki mbili, wapili laki moja na nusu na watatu laki moja pesa ambazo zimetolewa na Shirika la  Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC).


“Nimefurahi kuona mnajitoa na kushiriki katika mashindano kama hayo oneni wivu  kwa wenzenu walioshinda shindano ili mwakani mpate zawadi wengi zaidi naimani kupitia klabu zetu kuna vitu mnajifunza someni kwa bidiii masomo ya sayansi”  alisema Kyobya


Nae kaimu Afisa elimu halmashauri ya wilaya ya mtwara Shahara Shaibu alisema kuwa halmashauri hiyo imeweka mikakati ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapenda kusoma masomo ya sayansi.


“Ipo mikakati tumeweka ili kuhakikisha kuwa tunakamilia ujenzi wa maabala kujenga na kununua vifaa mwaka huu shule sita tutakamilisha zingine zitapangwa kwa awamu ijayo …Lakini zipo shule zina upungufu wa walimu tunao walimu wa makataba ambao wanatusaidia na tunawalipa ili kuweza kupunguza tatizo la uhaba wa wlaimu”


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo James Mataragio, Afisa Maenedeleo ya Jamii  wa Shirika hilo Ally MLuge  amewaasa wanafunzi kujitokeza katika mashindano kama hayo ili kujijengea uelewaa zaidi na kujiunga katika klabu za gesi asilia mashuleni ambazo zinaleta matokeo chanya.


“Uchumi wa gesi asilia ni uchumi mpana sana unagusa kila sekta ndio maana hadi majumbani tunnatumia gesi asilia, viwandani na sasa kwenye magari lazima tujitokeze na kuhamasisha zaidi wanafunzi kuifahamu na kupenda masomo ya sayansi kwa mustakabali wa Tanzania ya baadae” alisema Mluge


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI