Header Ads Widget

WAHITIMU 2,583 WATUNUKIWA VYETI NA LESENI ZA UUGUZI NA UKUNGA NCHINI.

 


Na WAF-DOM 


WIZARA ya Afya kupitia Baraza la Uuguzi na Ukunga imewatunuku Wahitimu 2,583 vyeti na leseni za Uuguzi na Ukunga kama ishara ya kuwa tayari kutoa huduma kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini. 


Akikabidhi vyeti hivyo leo Machi 26, 2022 katika ukumbi wa Chimwaga Jijini Dodoma, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe amewataka kuzingatia maadili na weledi kulingana na maelekezo ya Baraza la Uuguzi na Ukunga ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi. 


"Huduma bora ni zile zinazozingatia weledi na umahiri, maadili au uadilifu na kuwajali wagonjwa mara wanapofika katika maeneo ya huduma ili kuepuka malalamiko yanayoweza kuzuilika." Amesema Dkt. Sichalwe 



Nichukue nafasi hii kuwahimiza  kuzingatia miiko na taratibu zote mlizoelekezwa katika mafunzo, Sheria na Miongozo inayosimamia Taaluma  na kuwa mfano wa kuigwa na wanataaluma wengine. Amesisitiza 


Aidha, Dkt. Sichalwe ameipongeza Baraza kwa kuandaa “Kanzi Data” ambayo itawasaidia Wauguzi na Wakunga kuwa na taarifa sahihi zitakazosaidia katika mipango mbalimbali pamoja na kurahisisha huduma za kitaaluma zikiwemo maombi ya mitihani, Usajili, Leseni, uhakiki wa wataaluma na mengineyo. 





Mbali na hayo Dkt. Sichalwe amewataka Wauguzi na Wakunga kujenga tabia ya kujisomea mara kwa mara ikiwemo kujiendeleza kitaakuma ili kuendelea kuwa na ujuzi na umahiri kitaaluma kulingana na wakati na teknolojia (Continuing Professional Development).   



"Mnatakiwa kuhakikisha mnapata Mafunzo Endelevu ya Kitaaluma Kazini (Continuing Professional Development). Sayansi inabadilika magonjwa kila siku yanaingezeka,  nitoe wito kwenu kuhakikisha mnajiendeleza kitaaluma na kuwa na tabia ya kujisomea ili kupendana na kasi ya teknolojia." Amesema. 


Sambamba na hayo, amewaelekeza Baraza la Uuguzi na Ukunga kuendelea kuchukua hatua kwa Wauguzi na Wakunga ambao wanavunja Sheria na miiko ya taaluma bila kuwaonea ili wasiwachafue Wauguzi wengi wanaofanya kazi nzuri za kuwahudumia wananchi kwa kufuata maadili ya taaluma zao. 




Nae Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Bi. Ziada Sellah amewataka Wauguzi na Wakunga waliotunukiwa vyeti na leseni kwenda kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo ya kutoa huduma kwa kufanya kazi kwa bidii, uweledi na kujituma na kuacha kuwaza nafasi za uongozi. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI