Teddy Kilanga_Arusha
Mkuu mkoa wa Arusha,John Mongella amewataka vijana wa kike (Mabinti) kuendeleza bunifu zao katika kuisaidia serikali kutatua changamoto katika jamii.
Aidha Mongella amewasisitiza vijana hao wasichukulie tuzo za Chanya Change kama kitu rahisi kwani ni moja ya kigezo cha kuaminika katika taasisi mbalimbali hivyo ni vyema wakachukulia kama fursa ya kusonga mbele zaidi.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa vijana(Mabinti ) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini iliyofanyika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) na kuandaliwa na Taasisi ya Chanya Change,Mongella alisema suala la kujielimisha katika nyanja mbalimbali ni la msingi sana katika zama hizi za utandawazi
"Katika suala la kuchukua tuzo hizi katika maisha zina maana sana lakini licha ya hilo pia mnahitaji kujihimarisha zaidi kupitia nidhamu ambapo ndicho kila kitu ambapo itamsaidia binti kuepukana na vishawishi pamoja na ajali nyingi zilizoko kwenye dunia hii,"alisema Mongella.
Alisema tukio hilo ni darasa kwa watu wote pamoja na fursa ya kutafakari na kujitambua zaidi katika masuala ya ubunifu juu ya kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto katika jamii hivyo anaipongeza sana waandaji wa tuzo cha Chanya Change kwani imewaonyesha njia ya kupita kama serikali.
Jambo hili la vipawa vya ubunifu litasaidia mabinti na vijana katika kujitambua hivyo tunawapongeza sana uongozi wa chuo cha IAA kwa kuamua kuunga mkono suala la ubunifu ambalo linasaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
"Lazima mtu aweze kujitambua na kuthubutu kwani kuna watu wengi wanamawazo mazuri lakini wameshindwa kuthubutu nakushindwa kufahamu kuwa kitendo cha uthubutu kinamatokeo mawili kushindwa na kufaulu na hicho ndicho wengi wao wanashindwa kufahamu,"alisema Mongella.
Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Dk.Cairo Mwaitete alisema kitendo hicho cha utoaji wa tuzo kwa vijana wa kike ni jambo jema Mwalimu Pamela ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chanya Change ni mfano wa kuigwa kwani anawalea katika hali ya kunitegemea katika maisha yao.
"Jambo hili haliitaji mzaha katika kuandaa vijan wetu katika Taifa ambao watasimama na kujitambua kwenye Taifa lao ikiwa Taifa linanza kujengwa katika ngazi ya familia na kuwekea misingi iliyobora,"alisema Dkt.Mwaitete.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Chanya Change,Pamela Chogo alisema mchakato wa kuwapata washindi wa tuzo ulianza kwa washiriki kupendekeza majina yao pamoja na kutuma kazi zao kwa njia ya video ya kuonyesha kile wanachokifanya.
"Pia washiriki walipitia mchujo wa kuonana na majaji ambapo ulisaidia kupata washiriki walioshika nafasi ya tatu bora kwa kila eneo ikiwa lengo la utoaji wa tuzo ni kuwahimarisha na kuwahamasisha vijana wa kike katika kuifanya jamii wajifinze kutoka katika mabinti hao katika kutoa elimu ya masuala ya kupinga vitendo vya kikatili katika jamii,"alisema
Chogo alisema lengo linginr ni kuhamasisha matumizi chanya ya mitandao ya kijamii hivyo ni furaha yao kwamba zoezi hilo limetimia kwa kiasi kikubwa na kwa upande wa washindi Taasisi ya Chanya Change itaendelea kuwalea vijana hao kwa kuwapa mafunzo ya ushauri na malezi.
Aliongeza kuwa pia katika mchakato huo Taasisi ya Chanya Change iligundua kwamba vijana hao pamoja na kujitahidi kufikia malengo yao wengi wao wanashindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa mitaji pamoja na maarifa.
"Kwa sababu hiyo tunawaomba wadau wa Taasisi mbalimbali pamoja na serikali kuendelea kutupa ushirikiano ilo kwa pamoja kupata njia bora katika kuwasaidia vijana hawa na wengine wanaopitoa hali ya kutofikia ndoto walioianzisha,"alisem
0 Comments