Hamida Ramadhan Dodoma
WAKATI Serikali na wadau mabilimbali wakupinga ukatili wa kijinsia wakipambana katika huhakikisha vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto vinakwisha nchini,umeibuka ukatili mwengine kwa baadhi ya watoto wa jamii ya kifugaji kuwalawiti wanyama pindi wanapokuwa machungani.
wanyama wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kulawitiwa ambapo wadau hao wakupinga ukatili wamesema kunahaja ya kuwekeza nguvu kubwa kwa kuwalinda wanyama kwani viumbe hai hao wamekuwa wakifanyiwa ukatili kwa kulawitiwa
Akiongea na Kituo hiki,Mratibu kutoka Asasi ya Kigoma Woman Development Organization Decas Hulilo katika kikao hicho amesema matukio ya kulawiti wanyama kigoma yapo ambapo mwaka juzi alipata taarifa ya mwanafunzi wa darasa la 5 kutoka shule ya msingi ya Uhuru amekuwa akimlawiti Mbwa.
"Taarifa hizi tulizipata kwa walimu walezi wa clabu kwamba mtoto huyu awali alikuwa akiwaingilia wanafunzi wenzake baada ya kupigwa akaamua kuhamia kwa wanyama na siku aliyokuwa akimlawiti tuliitwa na tukaona mtoto huyo anatakiwa kupatiwa ushauri wa kisaikorojia,"
"Matukio kama haya yapo mengi tusiyafumbie macho wanyama wana haki na hawapasi kufanyiwa vitendo kama hivyo,"amesema Hulilo
Kwa upande wake,Mussa Jonas ni mwanaharakati wa kupinga vitendo vya kikatili Kutoka shirika la (TVMC) Mkoani Shinyanga na mjumbe wa (NACONGO) amesema kwa kipindi cha miezi mitatu katika mkoa wa Shinyanga matukio yaliosikika ya wanyama kulawitiwa na binadamu ni matukio 13 .
Amesema,watoto machungani wamekuwa wakiwalawiti Mbuzi,Kondoo na N'gombe ambapo amesema hali hiyo imekuwa kama mazoea na tabia kwa watoto hao.
Naye,Eveline Lyimo Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika linalojishughulisha kututea haki za wanawake na watoto walioko katika wilaya ya Ikungi kwa Kata 6 na Vijiji 18 amesema matukio ya kulawiti wanyama Mkoa wa Singida yapo kwa watu wazima na watoto ambapo jumla ya kesi 6 zimetambulika kesi 2 zikiwa ni za watu wazima na kesi 4 ni zawatoto.
Amesema,wumekuwa wakiwekeza nguvu kubwa kwenye kutetea ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ambao walidhani na kukiri kuwa ndio kundi lililopo hatarini kufanyiwa vitendo hivyo vya kikatili lakini kumbe wanyama nao ambao hawawezi hata kujitetea wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo vya kikatili.
Aidha,akielezea madhumuni ya kukutana katika kikao hicho Mratibu kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) anayetoka kwenye Idara ya Utafiti na Uchumbuzi Zainabu Mmari amesema ni kuangalia robo ya pili ya utekekezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kama njia mojawapo wa kutekeleza mpango kazi wa taifa wa kuthibiti vitendo vya ukatili kijinsia kwa wanawake na watoto nchini Tanzania .
Amesema,Mpango huo ulianzishwa mwaka 2016/2018 ni mpango wa miaka mitano na unaokadiriwa kuisha mwaka 2022 na katika kutekeleza mpango huo TGNP kwa kushirikiana na mashirika mengine ambayo yanapata ufadhili chini ya foundation for civil society (FCs) wamekuwa wakitekeleza miradi hiyo ya ukatili wa kijinsia kwa muda wa miaka mitano mfululizo kunzia mwaka 2017 hadi mwaka huu 2022 .
Amesema,kama kiongozi wa Kongani ya watu wanaopinga ukatili wa kijinsia wameweza kufanyakazi na mashirika zaidi ya 32 kutoka katika mikoa 14 ambapo 13 ni mikoa ya Tanzania bara na 13 Tanzania visiwani mikoa ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa na vitendo ya ukatili Hali iliyokuwa ikididimiza nguvu kazi na maendeleo ya nchi.
Hata hivyo,alivyoulizwa juu ya suala la ulawiti kwa wanyama amesema Jambo hilo amekuja kulisikia katika kikao hicho huku akisema kama jamii inatakiwa kupinga vitendo hivyo vya ukatili kwa wanyama kwa kuwaeleza watoto hao madhara wanayowasababishia wanyama na hata wao jinsi wanavyo athirika kisaikorojia kwa kufanya vitendo hivyo vya ukatili kwa wanyama .
"Tumesikia vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na watoto wadogo hasa wale wanaotoka katika jamii za kifugaji pindi wanapokuwa machungani wanalisha wanyama baadhi yao wamekuwa wakiwaingilia wanyama hao,"amesema.
0 Comments