Header Ads Widget

WAANDISHI WAASWA KUWA WAZALENDO

  

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuipenda nchi yao kwa kuwa wazalendo kwa kuandika habari ambazo zitajenga na sio za kugombana na serikali iliyopo madarakani badala yake watumie kalamu zao kusifia Nchi.Mwamdishi Pamela Mollel,MDTV Arusha


Rai hiyo ilitolewa machi 16/2022 na kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)Dkt Philibert Luhunga wakati akizungumza katika semina iliyowakutanisha waandishi,Watafiti na wabunifu Mkoani Arusha 



Alisema kuwa sio vyema waandishi kuandika vibaya kuhusu serikali badala yake watumie kalamu zao kuandika mazuri yanayofanywa katika nchi yao


"Pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo katika nchi ya Marekani huwezi kuskia wala kuona waandishi wa nchi hiyo wakikosoa serikali yao zaidi sana utaona wakitumia kalamu zao kusifia"Alisema Dkt Luhunga


Aliongeza kuwa ni vyema waandishi wakaisemea serikali ya Rais Samia Suluhu kwa mambo makubwa anayofanya katika Nchi hii


Pia aliwakumbusha waandishi hao juu ya umuhimu wa kujiheshimu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kujiweka nadhifu ili watu wengine waipende taaluma ya uandishi wa habari


Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka (COSTECH)Deusidedith  Leonard alisema kuwa lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika taarifa za Sayansi Teknolojia na Ubunifu kwa lugha rahisi ili ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka 

Alisema kupitia semina hizo wanategemea kupata ongezeko la makala pamoja na vipindi vinavyohusu Sayansi katika Redio,Televisheni,Magazeti na mitandao ya kijamii

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI