Header Ads Widget

VIJANA TOKA MAZINGIRA MAGUMU CHINI YA MRADI WA YAM KUWA KUCHANUA KIUCHUMI-MWANASAIKOLOJIA

Mwanafunzi wa Saikolojia chuo kikuu cha Iringa Germana Chuwa

IMEELEZWA kuwa upo uwezekano mkubwa wa mabinti na  vijana waliotoka kwenye mazingira magumu ambao walikata tamaa ya maisha Kuchanua kimaisha na kuwa na  mafanikio makubwa ya kiuchumi iwapo watakubali kubadilika .Mwandishi Francis Godwin,Matukio Daima Mufindi 

Hayo yameelezwa Leo  mwanafunzi wa Saikolojia kutoka chuo kikuu cha Iringa Germana Chuwa wakati wa warsha ya na  Saikolojia Kwa vijana 100 wanaotoka kwenye mazingira magumu kata tatu za Luhunga, Mdabulo na Ihanu wilayani Mufindi mkoani Iringa ambao ni wanufaika wa mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM)

Chuwa alisema vijana wengi toka kwenye mazingira magumu wameshindwa kusimama wenyewe baada ya kukata tamaa ya maisha kutokana na mazingira waliyokulia .


Ila alisema kupitia mradi huyo wa YAM na elimu ambayo wamekuwa wakipatiwa vijana hao watakuwa na mwango bora wa kutimiza ndoto zao ambazo walizikatisha kutokana na mazingira magumu waliyokulia.


Baadhi ya mabinti waliopata mimba utotoni wakiwa Katika majadiliano ya vikundi wakati wa mafunzo ya Afya ya akili

"Hawa vijana kutokana na mafunzo haya tunayoendelea kuwapa wameanza kuonekana ni vijana wenye shauku kubwa ya kupambana kuwa na maisha bora Kwa kumiliki uchumi wao hivyo wakitoka hapa Kwa mtaji wa elimu waliopata na wakiongezwa uwezeshwaji kiasi hawa watainuka Kwa kasi na hawataanguka tena"


Hivyo aliwataka vijana hao pindi watakapo maliza mafunzo ya siku 15 wanayopatiwa kusahau mazingira ya mwanzo na kuondoka na fikra mpya ya kwenda kupigania uchumi wao .


Mshiriki God Lumwesa ambae ni mlemavu wa viungo alisema kuwa kabla ya mafunzo hayo hakuwa na ndoto ya kuja kufanya shughuli yoyote zaidi ya kutegemea kusaidiwa Kwa Kila jambo huku akiamini yeye ni mlemavu asiyeweza kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi .


Lumwesa alisema Kwa Sasa amejipanga kurudi kuanzisha shughuli ya kiuchumi na kuisimamia ili kuja kuwa msaada Kwa familia yake .

Vijana toka mazingira magumu wakiwa Katika majadiliano ya vikundi wakati wa mafunzo ya Afya ya akili


Huku Leura Nyongole akielezea mafunzo hayo kama Kinga Kwa mabinti wenzake ambao hawakufanikiwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto ya kupata mimba  za utotoni .


Kwani alisema mabinti wengi walikata tamaa ya kusonga mbele kimaisha kutokana na kupata mimba wakiwa wadogo na Sasa kutokana na mafunzo hayo wanaamini watasonga mbele .


Mradi wa YAM unatekelezwa na   Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa Foxes  Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland na utakelekelezwa kwenye kata za Luhunga ,Ihanu na Mdabulo ni mradi utakaonufaisha  vijana na  watoto  wanaotoka  katika  familia duni zaidi ya   vijana 770  atika  vijiji 16.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI