Header Ads Widget

URUSI YASHAMBULIA UWANJA WA NDEGE WA LVIV.

 

Uwanja wa ndege wa mji wa Lviv leo umeshambuliwa na Urusi kwa makombora wakati ambapo nchi hiyo inapanua kampeni yake ya mashambulizi ya angani kote nchini Ukraine. Kampeni hiyo ya Urusi imepelekea kuibuka kwa madai ya uhalifu wa kivita na ulengaji wa maksudi wa raia. Meya wa mji wa Lviv Andriy Sadovyi amesema majeshi ya Urusi yamekishambulia kiwanda cha kukarabati ndege kilicho karibu na mpaka wa Poland. Kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa AFP moshi mkubwa ulionekana ukifuka kutoka katika uwanja huo wa ndege. Urusi imegeukia mashambulizi ya angani na masafa marefu kutokana na operesheni yao ya nchi kavu kukwama kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Ukraine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS