Header Ads Widget

DEREVA LORI LA MAFUTA KAMPUNI YA PANONE AFUNGWA JELA MIAKA MINNE NA FIDIA YA ZAIDI YA TSH MILIONI 16

MAHAKAMA ya  hakimu mkazi  mwandamizi wilaya ya Iringa  imemfunga jela  miaka  minne  pamoja na kulipa fidia ya shilingi milioni 16,050,000 aliyekuwa   dereva wa  lori la mafuta  la kampuni ya Panone And  Co. Ltd Faid Mussa  Manis  baada ya  kupatikana na hatia katika kesi jinai namba 2019 iliyokuwa  ikimkabili  yeye na  wenzake 6.


Akisoma  hukumu  hiyo jana hakimu mkazi  mwandamizi  wa mahakama ya hakimu mkazi  wilaya ya  Iringa  Emmy Nsangalufu  alisema kuwa  mahakama  hiyo   baada ya  kusikiliza  ushahidi  uliotolewa mahakamani  hapo pasipo  shaka  imejiridhisha  na  kuwatia kumtia hatiani dereva  huyo  na  wenzake   watano   kwa  kosa la  wizi  wa  kuaminika .

Washtakiwa  waliofikishwa mahakamani  hapo pamoja na  Manis ni  Abasi Seleman Finde  maarufu kwa  jina la Mchina , Frankl Manjir , Gerald John Mlelwa , Adam Kitururu Mzava ,Leonard Mwambela na Gaspa Juvenari Shirima.

 Alisema  kuwa  washtakiwa hao  walifikishwa mahakamani  hapo kwa makosa  matatu  ambayo ni kula  njama  ambalo  kosa  lililohusisha   washtakiwa  wote  saba ,kosa la  pili  ambalo llilimhusu  dereva  pekee ni wizi  wa  kuaminika  wakati  kosa la  tatu  lililowahusu  washtakiwa namba 2 na  7 ni wizi  wa  vitu  vya  kwenye  gari zikiwemo  lita 7200 za  mafuta .

Hivyo  alisema  kutokana na  ushahidi  uliowasilishwa  mahakamani  hapo  mahakama  hiyo  imemtia hatiani  kwa  kumfunga  jela  miaka miwili  dereva  Manis kwa kosa  la  kwanza la kula njama  na  kosa la  pili la wizi  wa kuaminika  inamhukumu  kifungo  cha miaka miwili na kufanya dereva  huyo  kutumikia  jela miaka  minne pamoja na  kulipa  fidia ya  shilingi  milioni 16 ,050,000.

Huku  mshtakiwa  namba 2 namba  4 ,6 na  7 wakikutwa na  hatia ya  kosa la  kuiba  vitu  vya  kwenye  gari hilo  ambapo  kila  mmoja atafungwa  jela  miaka  miwili  pamoja na kulipa fidia ya  shilingi milioni 16 ,050,000 za  mafuta  yaliyopotea  lita 7200.

Hata   hivyo  alisema  mahakama  hiyo  imejiridhisha pasipo  shaka   yoyote   na  kuwaachia  huru   washtakiwa  wawili kati ya  saba  ambao ni  namba   3  na tano  ambao  ni Frankl Manjir na Adam  Kitururu  Mzava   wakiachiwa   huru .


Katika   hukumu  hiyo   mahakama  hiyo  imewafupa washtakiwa   wanne  kati ya  watano  bila  kuwepo mahakamani  hapo  baada  ya  mmoja  kati  yao  kuruka  dhamana hatua  za  awali kabisa na  wengine  kutofika  kupokea  uamuzi  wa  hukumu  hiyo hivyo mahakama imeagiza  wasakwe na  wakipatikana   wapelekwe  gerezani.

Washtakiwa  hao  walikuwa  wakitetewa na  wakili Rwezaura Kaijage  ambae  aliomba  mahakama  hiyo  kuwapunguzia  adhabu   wateja  wake hao   huku upande  wa jamhuri   ukiongozwa na  wakili  Alice Thomas na  Jackline Nurga  ambao  waliiomba mahakama  hiyo  kutoa  adhabu  kali  ili  iwe fundisho kwa  watu  wenye tabia ya  kukosa  uaminifu  kwa mali  za  matajiri na serikali kwani   vitendo vya  wizi kama  huo  vimezidi  kuongezeka  nchini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI