Header Ads Widget

URUSI YASHAMBULIA JENGO LA MICHEZO.

Mamlaka nchini Ukraine zimesema vikosi vya Urusi vimeliteketeza jengo la michezo la mjini Mariupol ambalo inaelezwa kuwa na mamia ya watu walikuwa wanapatiwa hifadhi, kadhalika kuishambulia na miji mingine. Hayo yanatokea wakati pande zote mbili yaani Urusi na Ukraine, zikitoa makadiro ya matumaini katika mazungumzo ya amani baina ya pande hizo. Shumbulizi hilo lilipasua katikati jengo hilo, lililokuwa na watu ambao makazi yao yaliharibiwa na vita. Pamoja na kutofahamika kwa sasa idadi ya vifo au majeruhi lakini taarifa ilisema watu wengi walifukiwa na kifusi. Katika ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ameliita shambulizi hilo ni uhalifu mwingine wa kivita mjini Mariupol.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS