Header Ads Widget

WANANCHI KIJIJI CHA VISEZI WAMPA MATUMAINI RC KUNENGE

 


WANANCHI wa Kijiji cha Visezi na Kitongoji cha Kisogo wamemhakikishia mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge kuwa hawataukwamisha mradi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Vigwaza kwenda Kwala licha ya kutolipwa fidia.


Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho kwenye ya Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Kunenge alisema tayari mkandarasi amesimamisha ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 31.


Kunenge alisema kuwa serikali iko kwenye mchakato wa malipo kwa wale ambao hawajalipwa na unakaribia kufika mwisho hivyo hakuna sababu ya wananchi kupinga mradi huo wa barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha zege kwani unakwenda kufungua fursa za kiuchumi kwenye eneo hilo.



Kwa upande wake mkazi wa Kijiji hicho Magdalena Mpungu alisema kuwa wanashukuru ujio wa mkuu huyo wa mkoa na kukubali kutoukwamisha mradi huo lakini walipwe fidia zao mapema ili waangalie utaratibu mwingine wa maisha.


Naye Zaina Salehe alisema kuwa mradi anautaka lakini anachotaka ni kulipwa kwani kibanda anachoishi kitabomolewa na hana mahali pakwenda.


Said Kitala alisema wao wako tayari kupisha mradi lakini wawahishe malipo kwa wakati ili nao wakatafute makazi mengine na kufanya shughuli zao za maendeleo.


Awali mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Ally alisema kuwa ujenzi huo wa barabara umekumbwa na changamoto ambapo wananchi 109 hawajalipa fidia hivyo kutoa malalamiko yao.


Ally alisema kuwa eneo hilo limepakana Kijiji hicho na makazi ya wananchi na shamba la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo kuna mgogoro baina na wananchi na shamba hilo kwani inaonyesha ni eneo la serikali.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI