Na Ashton Balaigwa,Morogoro
Watu Sita wamefariki Dunia na wengine watatu kujeruhiwa kati yao wawili kulazwa katika Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro na mwingine katika Kituo cha Afya Dakawa baada ya gari dogo la abiria aina ya Noah waliokuwa wakisafiria kutoka Mji wa Dumila wilayani Kilosa kuelekea Morogoro mjini kugongana uso kwa uso na Lori lililokuwa kwenye masafa marefu kutokea Morogoro kwenda Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa huo, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotolea Mei 14, 2024 majira ya saa mbili asubuhi eneo la Dakawa ,wilayani Mvomero kwenye barabara kuu ya Dodoma- Morogoro.
Matukio Daima media tunatoa pole kwa wafiwa na kuwaombea Majeruhi wa ajali Afya njema
0 Comments