Header Ads Widget

UJUMBE WA STAA MONALISA BAADA YA MWANAE SONIA KUFANIKIWA KUTOKA UKRAINE

 


Na Andrew Chale 


STAA wa filamu za Kitanzania 'Bongo Movie' Yvonne Cherrie 'MONALISA'  ameandika ujumbe mzito kuonesha furaha yake na kuwashukuru wote waliokuwa wakimuombea mwanae aliyekuwa akisoma nchini Ukraine Taifa ambalo lipo kwenye vita kali dhidi ya Taifa jirani la Urusi ambayo inaendelea hadi sasa.


Monalisa ameonesha furaha yake hiyo ambapo pia amekerwa na maneno ya watu dhidi ya mtoto wake huku akinukuu baadhi ya jumbe mbaya kuhusu mwanae huyo.


Sonia ambaye ni binti mkubwa wa  Monalisa alikuwa anasoma Taifa hilo la Ukraine ambapo hivi karibuni pia alituma taarifa kuwa yupo salama huku akimtoa hofu mama yake huyo na Watanzania.


Jana Machi 8, 2022 Sonia na wenzake walifanikiwa kuingia nchi jirani ambapo kwa sasa taratibu za kurejea Tanzania zikiendelea.



Ujumbe alioandika Monalisa kupitia mitandao yake ya kijamii:



"Mungu wetu ametenda tena!!

Sasa, naweza kula chakula kikashuka, naweza kujilaza nikapata usingizi maana Binti yangu yupo salama nje ya mipaka ya nchi ya Ukraine."


"Alifanikiwa jana usiku kuingia nchi ya jirani yeye na wenzie wachache na wapo salama.


"Napenda kuwashukuru wote waliokuwa nasi katika kipindi kigumu ambacho tumepitia, hakika kilikuwa kipindi kigumu hasa,kama haukuwa na ndugu yoyote Ukraine ulikuwa unaona kama kichekesho tu kinachoendelea kwakuwa pengine sisi Tanzania (ikiwemo mimi mwenyewe) hatujawahi kujua hasa maana halisi ya neno Vita na tuendelee kuombea sana Taifa letu katika hili." 


"Kwa kipindi hiki, nimepata marafiki wapya hususani Watanzania waishio nje ya Tanzania nawashukuru sana.


"Lakini pia,nimepata kusoma comments ambazo sijawahi kusoma wala kuwaza binadamu anaweza kumuwazia binadamu mwenzie tena waziwazi kweupe.


"Mojawapo ni hii, "Putin mbona anachelewa kulipua bomu Sonia afe?" Huu ni zaidi ya uchawi.


"Ila comments hizi zinanifanya nizidi kuamini kwamba binti yangu ana kitu cha ziada na cha kipekee,na nikuambie wewe unaye 'comment' hivi usidhani unamuumiza bali unamjenga kuwa jasiri zaidi."


Shukrani zangu zote ni kwa Mungu pekee naamini hakika amefanya njia pasipo na njia, lakini kipekee niwashukuru wasanii wenzangu (baadhi) waliokuwa wakinipigia na kunipa moyo kwamba kila kitu kitakuwa sawa, viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu zangu hususani dada zangu, wazazi na rafiki zake Sonia, Media mbalimbali, Washarika wenzangu, wadau mbalimbali ninaofanya nao kazi, lakini Global Education Link mmetisha kabisa hususani kakaangu Abdulmalik Mollel"


Kwa wazazi wenzangu, ambao vijana wao ndio wapo safarini kuelekea Lviv ili waweze kuvuka kutoka nchi ya Ukraine, niwatie moyo kwamba vijana watavuka salama kwani Mungu wetu ni mkubwa. Shukran!" Aliandika Monalisa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI