Header Ads Widget

PSPTB WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA




 Na Hamida Ramadhan Dodoma 



NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango  Lawrence Mafuru ametoa wito kwa bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB) kusimamia Sheria iliyoianzisha bodi hiyo kwa kujumuisha usimamizi wa maadili,mienendo ya wataalamu na utengenezaji wa mitaala inayozingatia umahiri wa kitaalamu na mahitaji ya soko.


Akizungumza Jijini Dodoma Kwa niaba ya waziri wa fedha na mipango Dkt  Mwigulu Nchemba Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango amesema kuwa uandaaji na usimamizi wa miongozo mbalimbali inayohusu taaluma na kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu taaluma na kutoa majibu kwa changamoto zinazojitokeza kwenye taaluma hiyo.


Aidha amewaasa waajiri kutoa taarifa kwenye bodi zinazohusiana na ukiukaji wa maadili kwa wataalamu ili hatua sitahiki ziweze kuchukuliwa kwani hakuna ufanisi bila maadili na weledi.


"Hakikisheni waajiri wote wanaajiri watumishi wenye Sifa sitahiki zinazotambuliwa na Sheria ya PSPTB na kuzingatia mahitaji yaliyopo kwenye waraka wa Maendeleo ya utumishi namba 3 wa mwaka 2015 wa kada zilizopo chini ya Fedha na Mipango,"amesema Katibu.


Pia amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kusaidia bodi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na usimamizi mzuri wa Rasilimali watu pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali fedha ili malengo yaliyopangwa yaweze kutekelezwa kwa ufanisi


"Nawasisitiza kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanafanyakazi katika mazingira ya utulivu wa kutosha Ili waweze kutoa tija kwenye utendaji wao Mimi pamoja na viongozi wangu wa Wizara tunaimani kubwa kwenu katika kutekeleza haya,"amesisitiza Katibu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi PSPTB Jacob Jail Kibona amesema kuwa bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi,imepewa jukumu la kusimamia misingi ya taaluma ya ununuzi na Ugavi na mienendo ya wataalamu wake.


Aidha amesema kuwa bodi inawajibu wa kuzalisha wataalamu wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao.


"Bodi hii pia inajukumu la kuishauri Serikali kuhusu taaluma ya ununuzi na Ugavi Ili kuleta tija katika kutumia rasilimali za Serikali," .


"Naahidi kuwa bodi yangu itasimamia na kuimarisha taaluma ya ununuzi na Ugavi sambamba na kuongeza nguvu ya kupambana na vitendo vyote vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya ununuzi na Ugavi kama ubadhirifu wa Mali, Rushwa na ukiukaji wa taratibu za ununuzi na Ugavi,"amesema Mwenyekiti.


Hata hivyo Bodi ya wataalumu wa ununuzi na Ugavi imepewa jukumu la kusimamia misingi ya taaluma ya ununuzi na Ugavi na mienendo ya wataalamu wake,pamoja na kuzalisha wataalamu wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI