Header Ads Widget

MTU MMOJA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA KWA TUHUMA ZA KUMILIKI FUNGUO BANDIA 97.

 



Na, Titus Mwombeki-BUKOBA.


Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia bwana Furaha S/O Hansy mwenye umri wa miaka  58 mkazi wa jiji la Mbeya kwa kosa la kukutwa na funguo bandia 97 zikiwemo  funguo maalumu  nne (4) zenye uwezo wa kufungua mlango wa aina yoyote.


Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Wankyo Nyegisa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakwe na iliyopo mjini Bukoba.


“ Mtuhumiwa huyu amekamatwa katika wilaya ya Muleba akiwa hotelini na baada ya kukamatwa tumefanya naye mahojiano kuhusika kuhusika na matukio mbalimbali ya uvunjaji katika mkoa wa Kagera, Dar es salaam na jijini Mbeya”amesema kamanda Wankyo.


 Ameongeza kuwa jeshi la polisi mkoani Kagera limeweza kufanya operasheni ya wiki moja katika mji wa Bukoba na kuwakamata watuhumiwa 39 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya  mauwaji.


“Kuanzia tarehe moja(1) hadi tarehe tisa(9) mwezi Machi mwaka huu tulifanya operesheni na tumewakamata watuhumiwa mbalimbali kama vile watuhumiwa wa makosa ya mauaji, watuhumiwa wa kupatikana na Pombe haramu ya moshi(gongo) lita 87, mtuhumiwa wa wizi wa ng’ombe  20 pamoja na mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki”.


Aidha kamanda huyo wa pilisi ametoa rai  kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kuwa wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuachana na vitendo vya kiarifu. 


“Sisi tutarusha dawa kwa dawa jiwe kwa jiwe  popote pale waarifu watakapopatikana  katika mkoa wa kagera tutapambana nao ,wananchi lazima wafanye kazi kwa bidii Jeshi na kuachana na mambo ya kiharifu kwani  polisi mkoani kagera  tumejipanga vyema kukabiliana na waharifu  na atakayebainika  tutamshughulikia”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI