Header Ads Widget

NMB YAKABIDHI GUTA KWA MSINDI WA NMB BONGE LA MPANGO

 





NA HADIJA OMARY _LINDI.


BANK ya NMB kupitia kampeni yao ya bonge la mpango leo imemkabidhi mshindi wa kampeni hiyo  Badi Mohammedi mkazi wa Manispaa ya Lindi Mkoani humo  Guta aina ya Skaymark.



Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Stendi kuu ya Mabasi mjini Lindi Meneja wa kanda wa Bank hiyo janet shango alisema kuwa kwa kipindi kirefu sasa bank hiyo imekuwa ikiendesha kampeni ya NMB bonge la mpango yenye lengo la kutoa elimu kwa Wananchi namna ya kujiwekea akiba.



Alisema katika kampeni hiyo  fedha takribani Mlioni mia tatu ambazo zilikuwa zinashindaniwa  ambapo ikiwa ni  pesa taslimu ambazo zilikuwa zinatolewa kila wiki washindi 10 kiasi cha shilingi laki moja,  huku kila baada ya mwezi zikitolewa guta tatu



Aidha Bi. Shango aliongeza kuwa mpaka sasa katika Kanda hiyo ya Kusini jumla ya washindi 50 wa Guta za  Skaymark walipatikana ambapo kwa Mkoa wa Lindi ametokea katika manispaa hiyo.




Akikabidhi zawadi kwa Mshindi wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele alisema kuwa ni bahati ilioje kuona miongoni mwa washindi hamsini waliojishindia Guta zilizokuwa zikishindaniwa ni  Mteja kutoka manispaa ya Lindi , ambapo alimpongeza mshindi huyo kwa kushiriki Mashindano hayo



Mnwele alitumia fulsa hiyo pamoja na kumpongeza  mshindi huyo kwa namna alivyotumia fursa ya NMB kuweka Akiba kidogo kidogo  na hatimaye kuingia kwenye droo hiyo na kushinda pia  alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kutumia Bank hiyo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa.



Nae Meneja wa NMB Mkoa wa Lindi, Shabani Kasali alisema kuwa kwa Mteja anaetamani kushiriki katika kampeni hii anachotakiwa ni kuhakikisha anafanya miamala ya kuweka na kutoa kwa wingi . 



Kwa upande wake mshindi wa Guta Badi Selemani alisema kuwa ushindi huo umekuwa kama bahati kwake kwani hata alipokuwa akitumia Bank hiyo kwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa akutarajia kama angeingia kwenye  droo ya mashindano hayo.




“ nilishangaa kwa siku chache zilizopita kupigiwa simu kwa mtu aliejitambulisha kama ni afisa kutoka Bank ya NMB kuniambia kama nimeshinda Guta kwa kweli sikuamini nilidhani kuwa ni Matapeli ila ilipofika siku ya jana kuambiwa leo nitakabidhiwa Guta yangu kwa kweli nimefurahi sana sana” alisema Badi



Hata hivyo akielezea furaha yake Badi alisema zawadi hiyo imefika wakati muafaka kwa kuwa yeye kwa Sasa ni msaafu  ambapo atalitumia Guta hilo katika shughuli zake za Shambani kubeba mzao yake



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI