Header Ads Widget

HUDUMA ZA MAJI MTAMA ZAIMARIKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 90

 



NA HADIJA OMARY _LINDI.


Huduma  za upatikanaji wa maji safi na salama katika kata za Pangatena,  Namangale na  Nyangamara halmashauri ya mtama mkoani lindi zimeimarika kwa Zaidi ya asilimia 90 kwa kipindi cha miaka mitatu  mfululizo 2020 -2022



Hayo yamebainishwa na afisa mradi wa ufuatiliaji wa rasilimali za uuma , unaofanywa katika miradi ya maji halmashauri hiyo ya Mtama  karimu Mnedi alipokuwa akieleza mafanikio ya Mradi huo katika kikao   kilichofanyika katika kata ya Nyangao chenye lengo la kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mradi huo .



Mradi huo wa Kuimarisha Uwezo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma kwa Jamii katika  Sekta ya Maji  Halmashauri ya Mtamaunatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la RONDO WOMENS DEVELOPMENT ORGANIZATION (ROWODO) kwa ufadhiri wa foundation for civil society (FCS)



Mnedi alisema uimarikaji huo umetokana na jitihada mbali mbali zilizofanya na shirika ilo ikiwa pamoja na Kufanya Ufuatiliaji wa Ukarabati mkubwa wa miradi 3 ya maji , mradi wa Namangale, Pangatena na Nyangamara  pamoja na changamoto za uendeshaji wa miradi ya Maji katika kata hizo



Kuendesha  Mafunzo  juu ya usimamizi na utekelezaji wa pamoja wa sera na sheria Na. 5 ya Maji ya mwaka 2019 pamoja na Ufuatiliaji wa rasilimali za umma ili kuwa na miradi endelevu pamoja na Ufuatiliaji na Tathimini ya shughuli za Mradi



“Tumeweza kufikia malengo ya Kuimarisha huduma za upatikanaji wa maji  kwa sababu  wakati tunapokea mradi 2019  Mfano kwenye mradi wa maji ya Pangatena ambapo tangu kumalizika kwa shughuli za mkandarasi  katika Mradi huu uliogharimu Mil 980 Hali ya Upatikanaji maji ilikua duni kiasi cha  mradi kupewa sifa ya kuwa mradi kichefuchefu lakini kwa hivi sasa maji yanapatikana muda wote” alifafanua Mnedi



Hata hivyo Mnedi alieleza hali ya upatikanaji wa maji kabla ya mradi  na sasa ambapo katika kata ya pangatena imeongezeka kutoka  asilimia 40 mwaka 2020 mpaka kufika asilimia  93, namangale kutoka asilimia 63 mwaka 2020 mpaka kufikia 95 mwaka 2022  huku nyangamara ikionezeka kwa asilimia 94 mwaka 2022 kutoka asilimia 78 mwaka 2020.




Nae Afisa kutoka Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) Mhandusi Nasoro Mohamed, alisema kuwa  tangu shirika hilo la  Rowodo lianze  kushirikisha Wananchi kulinda na kusimamia miradi yao  katika kata hizo mabadiliko makubwa yameanza kuonekana ikiwa pamoja na mapato yanayotokana na miradi hiyo kuongezeka, kupungua kwa migogoro na miradi kuwa endelevu.



"Sisi kama  Ruwasa sasa tunajivunia ROWODO kwa sababu uendelevu wa vituo vyetu vya maji kwa maeneo yenye mradi  umeongezeka kwani hapo awali unaweza kukuta  kituo kimoja hakifanyi kazi kwa muda mrefu  hata kwa miezi mitatu  lakini kupitia Rowodo ile taarifa ya haraka tunaweza kuipata hivyo tunaishukuru Rowodo kwa ufuatiliaji wa karibu katika miradi hii na pia tunawaomba kama watakuwa na miradi mingine basi uwezo huu ujengwe hata katika kata zingine" alisema Mhandisi Nasoro



Akifunga kikao hiko muwakilishi wa katibu Tawala Wilaya ya Lindi ,  katibu Tarafa halmashauri ya Mtama, Mudhihiri Njonjoro pamoja na kulipongeza shirika la ROWODO kwa kuwajengea  uwezo  wananchi wa  kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma katika sekta hiyo  ya maji lakini pia alisema jambo linalofanywa na shirika hilo ni Dopromasia



"Alisema ingawa wananchi wanadhani Dipromasia  inahusisha mahusiano ya Nchi na Nchi lakini hata hili linalofanywa na Rowodo la kutatua migogoro na hata upatanishi kwa wananchi na jumuia za watumia maji ni moja ya kazi ya kidipromasia" 




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI