Header Ads Widget

MEYA WA MANISPAA YA SONGEA AWATAKA MADIWANI KUFANYA MABONAZA KWENYE KATA ZAO.

 



Na Amon Mtega _Songea.


MEYA wa  Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Michael Mbano amewataka Madiwani wa Manispaa hiyo kuandaa mabonaza ya michezo mbalimbali  kwenye kata zao ili kuibua vipaji vya michezo kwa vijana waliopo kwenye kata hizo.


Wito umetolewa na Meya huyo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye bonaza lililoandaliwa na diwani wa kata ya Ndilimalitembo Issa Chiweneke ambalo limekuwa maalumu kwaajili ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii kutoka na utendaji wake wa kazi katika Jimbo hilo.


Mbano akitoa zawadi mbalimbali kwa washindi wamashindano ya  bonaza hilo amesema kuwa kuna kila sababu kwa kila diwani kuona namna ya kuandaa mabonaza hayo kwenye kata zao na kuwa licha kuibua vipaji kwa vijana lakini bado michezo hiyo huwaburudisha Wananchi ambao ni wakazi wa kwenye maeneo yao wanayoyaongoza.



 Aidha meya huyo kupitia malengo ya bonaza hilo ametoa pongezi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan pamoja Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi pamoja na kuendeleza michezo mbalimbali kwa vijana wa Songea na Nchi nzima kwa ujumla.


 Hata hivyo Mbano amewapongeza Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA)pamoja na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SOUWASA)kwa kushiriki kikamilifu bonaza hilo ambapo timu zao za mpira wa miguu zilionyesha ushindani mkubwa kwenye bonaza hilo.



Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ndilimalitembo Issa Chiweneke amesema kuwa alifikia maamuzi ya kubuni bonaza hilo ambalo la kuipongeza Serikali pamoja Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro baada ya kuona kazi za utekelezaji wa miradi mbalimbali zinazofanyika ndani ya Manispaa hiyo .

 

 Naye mwakilishi wa Souwasa katika Manispaa ya Songea ,Abely Ngilangwa amesema kuwa wameshiriki Bonaza hilo kikamilifu ikiwa ni sehemu ya kutambua kazi zinazofanyika na Serikali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt, Damas Ndumbaro .




 Ngilangwa ambaye ni mwanasheria wa Souwasa amesema kuwa licha ya kutambua kazi zinazofanyika na Serikali lakini bado Mamlaka ya maji imetumia nafasi hiyo kutangaza utendaji kazi wa mamlaka hiyo ikiwemo na kuelekea kwenye wiki ya maji .

         

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI