Mapenzi ni kizunguzungu ,mapenzi yana Siri nzito na mapenzi hayachagui nani wa kumpenda naweza kuanzia hapa Leo.
Mzee Augustino Lyatonga Mrema si Mzee wa kwanza kuuthibitishia umma pasipo shaka kama yote wasemayo Kuhusu mapenzi yana wezekana kabisa na kwenye mapenzi hakuna umri wa kupenda Bora mradi huyu umpendaye ni zaidi ya miaka 18.
Ifahanike kuwa ndoa ni makubaliano ya watu wawili kwanza kabla ya kuhusisha wazazi ama Viongozi wa dini Kwa maana ya lufungisha ndoa .
Kama hivyo ndivyo basi Mzee Augustino Lyatonga Mrema amezingatia yote Kwa uadilifu wote na yeye amekwenda mbali zaidi Kwa kiutangaza ndoa yake kwenye vyombo vya habari ili umma wa watanzania na Dunia ijue.
Jambo hili si wengi wanafanya ila Mrema kafanya Kwa uwazi zaidi na hata kuuthibitishia umma kuwa ndoa yake haina pingamizi lolote nani naungana na Mzee Mrema kuwa binti aliyemchagua ni binti mbichi kabisa na hajawa na michepuko ndio maana toka atangaze hakuna pingamizi zaidi ya pongezi na mshangao mkubwa .
Mshangao wa umma unakuja tu umri wa Mzee Augustino Lyatonga Mrema na binti mbichi bibi harusi mtarajiwa lakini umaarufu wa Mzee Augustino Lyatonga Mrema uliotaka kusaulika njisi tukio Hilo lilivyomsogeza kwenye vinywa vya wengi .
Wapo wanaofikiri Mzee Augustino Lyatonga Mrema ameamua kutumia njia hiyo kufanya Siasa na wapo Wanaosema Mzee Augustino Lyatonga Mrema ametaka kuonyesha umma kuwa penzi Lina Siri nzito na siku zote tafuta pesa mabinti wabichi watakutafuta na usikombilie kutafuta mabinti Wazuri huku mfukoni huna pesa .
Japo wapo akina mama wenye umri wa Mzee Augustino Lyatonga Mrema ambao wameamua kujipatia vijana wadogo zaidi hii ni wazi kwenye maisha Kila mmoja anachagu mtu wa kuishi nae ukiacha wale wanaofuata Mali ila wengi wanaamini kuoa /kuolewa na Mzee hakuna stress za ndoa maana hapo alipo amefika atoke aende wapi Bora tu wewe umri wa Saa sita kujituliza uliposhikwa.
Hata hivyo zipo taarifa ambazo zinaenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Binti mwanafunzi wa CBE ambae picha yake inasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anaolewa na Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kukanusha kuwa hafungi ndoa na Mrema na wala hawawahi kuonana na Mrema na Hana makubaliano yoyote ya kufunga ndoa ataka umma upuuze taarifa hizo.
0 Comments