Header Ads Widget

WAZIRI DKT. DAMAS NDUMBARO AWATAKA WATANZANIA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA

 



Na Amon Mtega, Songea 


WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt ,Damas Ndumbaro amewataka Watanzania kuungamkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Maliasili na Utalii ili kuendelea kukuza uchumi wa Tanzania.

 

 Wito ameutoa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya Mkoani Ruvuma juu ya mafanikio yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya mwaka mmoja wa madaraka yake katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Maliasili na Utalii.


 Dkt Ndumbaro akizungumzia mafanikio katika sekta ya Maliasili na Utalii amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi kwenye sekta hiyo ikiwemo kujitolea kutangaza utalii kwa kuwaongoza watalii jambo ambalo halijawahi kufanywa na Rais yeyote Duniani.




 Amesema kuwa kufuatia hali hiyo Watanzania wanatakiwa kuendelea kuungamkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ili mwisho wa siku uchumi wa Tanzania uendelee kusongambele zaidi.

 

 Waziri Ndumbaro amefafanua kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais  huyo watalii wameongezeka wakiwemo wa ndani asilimia 40.2 na wa Nje asilimia 48 jambo ambalo limefanya mapato yaongezeke toka Sh.Bilioni 9.7 hadi Sh.Bilioni 12 .4 .


  Aidha amesema kuwa licha ya kuongezeka kwa mapato hayo lakini bado kumekuwepo na ongezeko la Wanyamapori kama Faru ambao wamefikia idadi ya takribani 200 huku Simba nao wameongezeka na kuwa asilimia 64 Duniani Simba wapo Tanzania.


  Hata hivyo amesema kuwa kutokana na usimamizi imara ujangili umepungua kwa asilimia 90 jambo ambalo linafanya Wanyamapori waendelee kuzaliana kwa wingi kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo.


 Pia amesema kuwa Serikali  ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuziboresha sekta mbalimbali hapa Nchini ikiwemo ya Maliasili na Utalii hivyo katika sekta ya Maliasili na Utalii Watanzania wategemee mabadiliko zaidi.

       


   

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI