Shirika la Maendeleo ya Jamii na Misitu kanda ya Kitapilimwa (MJUMIKK), kupitia mradi wa ufuatiaji na uhajibikaji wa Jamii (SAM) Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa imefuatilia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali na wadau katika kata za Ilolompya, Mlenge, Masaka na Kiwere na kubaini baadhi ya changamoto.
Akizungumza jana wakati wa mkutano wa mrejesho wa shughuli za kamati ya SAM wilaya Iringa, Katibu Mkuu wa shirika la MJUMIKK, Mashaka Kilanga amesema kuwa baadhi ya vijiji vya kata hizo tajwa vina miradi mbalimbali ya kilimo inayotekelezwa hususani umwagiliaji, maghala na mashine za kukoboa mpunga.
Alisema kuwa kamati hiyo imebaini mambo kadhaa ambayo yanaweza kupunguza ufanisi ama tija kwa wakulima ili kutokemeza umasikini na njaa.
Kilanga aliongeza kuwa miongoni mwa mamabo hayo ni kama vile ukosefu wa mashine ya kukoboa mpunga katika ghala la Mlenge unaopelekea wakulima kuongeza gharama za usafirishaji mazao yao sehemu zilizo na maghala na mashine za kukoboa.
Kukosekana kwa miundombinu rafiki ya kuanikia mpunga pia unakwamisha ufanisi rafiki kwa ghala la Mlenge na pia ukosefu wa ushirika madhubuti unaweza kupunguza tija kwa wakaulima kuweza kuongeza ufanisi wa ghala.
Kamati ya SAM Wilaya ya Iringa imejikita katika kufuatilia ufanisi wa miradi tajwa kwa lengo la kuongeza tija kwa wananchi, ambalo ni lengo kuu la serikali kukuza uchumi wa wakulima katika maeneo yao.
Kamati hiyo imejengewa uwezo wa kufuatilia miradi katika sekta mbalimbali kwenye jamii kwa ufadhili wa taasisi ya ‘The Foundation for Civil Society (FCS)’.
“Kamati hii imekuwa ikiomba ‘U3’ kutoka kwa watoa huduma wa sekta mbalimbali za umma ili kupata, Ufafanuzi, Uthibitisho na Uhalalalisho (U3), yote hayo ya kilenga kuona kuwa jamiii inapata kile kilichokusudiwa na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo,” alifafanua Kilanga.
Pia kamati ya SAM imepongeza serikali, Shirika la Chakula Duniani (FAO) pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwezesha wakulima wa kata za Ilolompya, Masaka, Mlenge na Kiwere wilayani Iringa.
Aidha, kamati ya SAM Wilaya ya Iringa katika utekelezaji wa majukumu wanakubana na changamoto ya ucheleweshaji wa upatikanaji wa takwimu toka kwa wataalamu wa halmashauri ya wilaya na kusababisha kukosekana kwa baadhi ya taarifa kamili wakati wa mkutano wa mrejesho wa shughuli za ufuatiliaji waliofanywa na kamati hiyo.
Naye, Diwani wa Kata ya Ilolompya katika tarafa ya Pawaga, Fundi Mihayo aliupongeza mradi wa SAM kwa kushughuli za ufuatiliaji wa miradi inayotekekezwa katika maeneo yao, lakini akatoa angalizo kwa kamati hiyo kushirikisha wadau muhimu wakati wa ufuataliaji.
Alisema kuwa kuwa kabla ya kamati ya SAM haijawasilisha taarifa hiyo kwenye mkutano wa mrejesho, watitahidi kuwaona watu wanahusika ili kuzifanya taarifa hizo kuwa bora Zaidi.
Mihayo aliomba kamati hiyo ishirikesha pia wajumbe wa kamati za maendeleo za kata (WDCs) ili kuweza kutatua changamoto ambazo zinaweza kutatulia katika ngazi ya kata na zile zinahusu halmashauri zipelekwe huku zikapatiwe majawabu.
Naye diwani kata ya Masaka Mathew Zanyagwa ameshauri serikali ionehaja ya kuanzisha wakala wa tume ya umwagiliaji ngazi ya halmashauri kama ilivyo kwa barabara (TARURA) na maji (RUWASA), ili iweze kusimamia shughuli za umwagiliaji kwa ukaribu.
Alisema kuwa tume ya umwagiliaji taifa ipo jijini Dodoma na inamtumishi wake mmoja ngazi ya mkoa wakati ngazi ya wilaya hayupo.
Zanyagwa alifafanua kuwa tume hiyo haina mahusiano ya karibu na halmashauri na kusababisha miundombinu ngazi ya halmshauri kutofanya vizuri ikizingatia wataalamu wote hapo wilayani.
Aliongeza kuwa kuwepo kwa wakala hao kutaongeza ufanisi ama tija kwa wakulima na hatimaye kutokemeza umasikini na njaa.
Kwa upande wake, Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Dorah Mlomo amesema kuwa mradi wa Uajibikaji na Ufuatiliaji Jamii (SAM) katika masuala ya umwagiliaji na uboeshaji wa mazingira unasaidia katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zinatakiwa kufuatiliwa ili shughuli zao zisiharibu mazingira.
Mlomo ametoa rai kwa jamii kujikita katika kuhakikisha miundombinu ilyojengwa na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo inatumika ipasavyo, ikiwemo miundombinu ya umwagiliaji katika kata za Mlenge, Masaka, Ilolompya na Kiwere.
Aliongeza kuwa miundombinu yote lazima itunzwe na kuheshimiwa na wakulima na wafugaji ili maji yaweze kupatikana kwa ajili ya shughuli za kilimo.
0 Comments