Na Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kusimamia na kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya juu ili kuendelea kukidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Alitoa maagizo hayo leo Juni 20, 2025 alipomwakilisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro(MUM), kwenye viwanja vya chuo hicho mkoani hapo.
Alisema.“Mamlaka zetu ziendelee kusimamia hilo kwa kufanya hivyo sio tu kutaendelea kukuza ubora wa elimu yetu, bali pia kutawawezesha wasomi nchini kukidhi viwango na mahitaji ya soko la ajira”.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka Taasisi za Elimu nchini ziimarishe mahusiano na vyuo vyote nchini vinavyotoa maarifa kwa vijana wa kitanzania pamoja na kuzalisha wakufunzi ili kuwa sehemu ya mtandao wa utoaji maarifa na taalum hapa nchini.
Waziri mkuu Majaliwa alisema kuwa katika kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya chuo hicho kupitia mfumo maalum wa (MUM Community Fund),ambapo Rais Samia ametoa kiasi cha Sh milioni 100 ili kiendelee kutoa huduma kwa watoto wa Kitanzania na yeye binafsi akachangia sh milioni 10.
Aliongeza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa Mfumo wa Takwimu wa Sekta ya Elimu utakaowezesha upatikanaji wa takwimu zote za sekta hiyo ambao utakuwa na uwezo wa kupokea takwimu mbalimbali zinazohusiana na elimu kutoka katika mifumo mingine ya Serikali ikiwemo NIDA, RITA na Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ,Omar Kipanga alisema kuwa katika kipindi cha miaka 20, chuo hicho kimefanikiwa kuwa na progrma zaidi ya 32 kutoka program mbili wakati kinaanza na kimefanikiwa kutoa wahitimu zaidi ya 15,000.
“Wahitimu hawa wamekuwa wwamekuwa wa kupigiwa mfano katika kazi na maadili inayofanya waaminiwe katika nafasi mbalimbali kwenye jamii na Serikali kaa ujumla”alisema.
Kadhalika, aliongeza kuwa Chuo hicho kimeweka mipango inayozingatia dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 na mwelekeo mpya wa Elimu Nchini Tanzania unaolenga kutoa Elimu Ujuzi, Stadi na Maarifa kwa ajili ya kuwajengea wahitimu uwezo na sifa za kujiajiri na kuajirika katika soko shindani la ajira duniani.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Waislamu (MDF),Dk Ramadhani Dau alisema Bodi na uongozi wa Chuo Kikuu hicho inamshuuru Rais wa Awamu ya Tatu , Benjamin William Mkapa kwa uamuzi wake wa kuwakambidhi majengo yaliyokuwa Chuo cha Tanesco mwaka 2005 ili kuanzisha chuo Kikuu hicho.
Naye Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dk Abubakar Zubeir bin in Ali alitoa wito kwa Waislam na Watanzania kwa ujumla kuweka mikakati ya kukisaidia chuo ili kiendelee kufanya vizuri na kutoa elimu kwa watanzania nchini.
“Waislam na watanzania tukisaidie chuo hichi, hakuna uislam bila ualimu, uislam ulipokuja ulipiga sana vita ujinga, tuwaunge mkono viongozi wetu kwa kukisaidia chuo hiki”alisema.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Mussa Assad amesema kuwa moja ya changamoto kubwa katika chuo hicho ni kukosekana kwa hosteli za wanafunzi wa kike “Namna tunavyoingeza udahili ndivyo tunavyoibua changamoto nyingine, tunataka watoto wetu wa kike wote wake ndani ya chuo”
Mwisho.
0 Comments