Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.
Meneja wa Tanroad mkoa wa kagera ametakiwa kuwasilisha taarifa ya namna ya kupunguza mpando wa barabara ya Nyangoye ndani ya miezi miwili ilikupunguza ajari na vifo ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara kutokana na barabara hiyo kuwa na mpando mkali .
Kauli hiyo imetolewa na mkamu mkuu wa rais Dkt. Philip Mpango katika mkutano wa adhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa wa Mayunda uliopo halmashauri ya manispaa ya Bukoba mkoani wa Kagera baada ya mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Steven Byabato kumuomba makamu wa rais kutatua changamoto ya barabara hiyo kwani imeleta madhara makubwa ikiwemo wananchi kupoteza maisha.
“Ninatoa miezi miwili tu kwa meneja wa tanroad taarifa ya barabara ya Nyangoye iwe iweimeshatolewa hasa ya jinsi ya kupunguza mpando mkali na kona kali ya barabara hiyo, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suruhu Hassan inawapenda wananchi wake hasa wananchi wa Kagera hivyo imejipanga sana kuhakikisha inatatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Tanzania ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara” amesema Dkt.Mpango.
Aidha makamu wa rais amesema kuwa, amepokea maombi yote yaliyotolewa na viongozi wa mkoa mkoa huo hasa la kuwepo changamoto ya ubovu wa stendi ya mabasi ambayo imeonekana kuwa changomoto kwa muda mrefu.
“Najua kuwa kuna changomoto mbalimbali kama zilivyotajwa na baadhi ya viongozi hasa mbunge wa jimbo hili, niseme kuwa serikali tayari imetenga shilingi bilioni moja katika mwaka wa fedha 2022/2023 ya kuanzia ujenzi wa stendi mpya naya kisasa ya inayotarajiwa kujengwa katika eneo la Kyakailabwa”.
Sambamba na hilo Dkt. Mpango amewasihi wananchi halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kupanda miti kwa wingi ili kupendezesha mji wao.
0 Comments