Header Ads Widget

ENG. KUNDO ATANGAZA KUGOMBEA JIMBO LA BARIADI MJINI.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025, atagombea Jimbo la Bariadi Mjini badala ya Jimbo la Bariadi vijijini kama alivyokuwa ametangaza awali.


Itakumbukwe kuwa hivi karibuni, Mbunge huyo alitangaza kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Jimbo la Bariadi, lakini amesema kuwa hatagombea na badala yake amemwachia Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa.


Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji ameyasema hayo leo kwenye Mikutano ya hadhara ya kuwasilisha Ilani ya CCM (2020/2025) iliyofanyika katika kata za Bunamhala na Isanga kwenye Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


"Kaka yangu nae alisema anagombea Jimbo la Bariadi, tukigombea wote matokeo yake  unakiktakata Chama..mtu akikuzidi umri ni kaka yako, hekima na busara zilinitawala, mimi nimerudi mjini,...siwezi kusababisha mipasuko ndani ya CCM, na tukakubaliana yeye abaki vijijini." Amesema na kuongeza.


" Nafasi za kugombea kwenye Chama Cha Mapinduzi, ziko chini ya CCM...hivyo tunafuata maelekezo ya Chama."


Akiwa kata ya Bunamhala, Mhandisi Kundo amesema kuwa serikali amewataka wananchi kuendelea kusimamia CCM kwami imetekeleza miradi mingi ya Maendeleo katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa VETA, miradi ya Elimu, Maji na Umeme.


Pia amekabidhi Mipira 52 kwa ajili ya Mitaa 13, kila mtaa umepata mipira 4 na jezi pea moja kila mtaa huku kata ya Bunamhala ikikabidhiwa mipira 3 na jezi pea 1.


Akiwa kata ya Isanga, Mhandisi Kundo amesema serikali ya CCM chini ya Rais Dkt. Samia imetekeleza miradi ya Maendeleo ya zaidi ya shilingi Bil. 1 katika sekta za Elimu, Maji na Umeme.


Amesema atahakikisha kata hiyo inafunguka kwenye mawasiliano hasa kufanikisha ujenzi wa Barabara ya Kidinda-Isanga-Wala ili iweze kupitika muda wote.


"Serikali tutaendelea kuboresha miundombinu ii ifikike muda wote, tutahikisha Umeme ili watu wafanye Biashara muda wote na Vipaumble vyangu ni miundombinu (Umeme, Barabara, daraja) ili kurahisisha utoaji wa huduma" amesema Mbunge huyo.


Amekabidhi mipira 35 kwenye Mitaa 8, ambapo kila mtaa umepata  mipira 3 na pea moja ya jezi huku  kata ya Isanga ikikabidbiwa mipira 3 na jezi pea 1.


Mwisho. 


















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI