Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROF PATRICK NDAKIDEMI ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA MAJI KATA YA URU MASHARIKI

 



NA WILLIUM PAUL,  MOSHI. 

Mbunge wa jimbo la Moshi  Vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof Patrick Ndakidemi amesema serikali imeendelea kutoa fedha ili kuhakikisha tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama linakoma.


Hayo aliyabainisha jana alipoongozana na madiwani wa Kata ya Uru Mashariki Samwel Materu na Delina Temba, diwani wa Kata ya Shimbwe Bertin Mkami, Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu kutembelea na kukagua Mradi wa maji Kata ya Uru Mashariki unao pata maji kutoka kata ya Uru Shimbwe na  hudumia vijiji vya Mnini na Mamboleo.



Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (Muwsa) mhandisi Kija Limbe alieleza kuwa mradi huo wenye thamani ya milioni 386 unatekelezwa na MUWSA na unategewewa kutatua kero ya uhaba wa maji unaokabili wananchi waliopo eneo la mradi.



Baada ya kukagua  mradi, mbunge alizungumza na wananchi katika kijiji cha Mnini ambapo alisema kuwa, serikali imetoa fedha za kutatua kero ya maji.


Alisema kuwa,  mbali na mradi huo wa maji pia imetoa fedha kwa miradi mingine ya maendeleo katika kata hiyo ikiwamo ujenzi wa daraja la Rau lililogharimu milioni 910 na kwa sasa limeshakamilika na linapitia.


"Nimshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu Hasani kwa jinsi ambavyo amekuwa akituletea fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo tunajukumu kubwa la kuhakikisha tunamuunga mkono kwa vitendo na kufanya kazi kwa bidii" alisema Mbunge Prof. Ndakidemi. 



Mbunge huyo alitumia pia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuilinda na kuitunza miradi inayoleta na serikali ili iweze kudumu kwa muda mrefu. 


Naye Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhan Mahanyu alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kuwaunga mkono viongozo pamoja na chama kwa jinsi wanavyopambana kutatua kero za wananchi.


Alisema kuwa ni kipindi kifupi tangu viongozi hao kuchaguliwa na kuingia madarakani lakini wamefanya kazi kubwa zinazoonekana kwa wananchi. 


Katibu huyo pia alisisitiza wananchi kuona umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji hayakauki. 


Mwisho... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI