Header Ads Widget

MBUNGE PROF. NDAKIDEMI AKABIDHI AHADI YAKE YA SARUJI MIFUKO 70"



NA WILLIUM PAUL,  MOSHI.

MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro,  Prof. Patrick Ndakidemi ametimiza ahadi yake ya kutoa saruji mifuko 70 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya wauguzi wa zahanati Tema kata ya Mbokomu. 


Mbunge huyo alitoa ahadi hiyo alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi wa nyumba hiyo ambapo saruji hiyo ilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Tema, Flex Macha, viongozi wa Ujenzi, Diwani wa kata ya Mbokomu Rafael Materu pamoja na msimamizi wa Zahanati na wananchi wengine wa kitongoji C.



Akizungumza kwa  niaba ya Wananchi Mwenyekiti wa Kijiji, Ndugu Flex Macha amemshukuru Sana Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini  kwa kutimiza ahadi yake.



"Tunamshukuru Sana Mbunge kwa kutimiza ahadi yake leo hakika tumefarijika sana kwa mchango wake, tutasimamia kikamilifu mchango wake" Alisema Mwenyekiti. 


Naye Diwani wa kata hiyo Raphael Materu kwa niaba ya Wana Mbokomu ameendelea kumshukuru Mhe Mbunge kwa kuendelea kuipigania kata yake katika Mambo ya maendeleo.



"Mhe Mbunge amekuwa akitupigania katika vitu vingi, na niseme tu kuwa amekuwa akinipa ushirikiano kila wakati tunashukuru sana Ofisi ya Mbunge kwa niaba ya Mbunge kwa kuwasilisha ahadi ya saruji takribani mifuko 70" Alisema Diwani. 



Katika ahadi hiyo Mbunge aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni moja na amefanya hivyo.

Mwisho....

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI