Header Ads Widget

HAWA HAPA WASANII WATAKAO NOGESHA SAMAKI FESTIVAL JUMAMOSI YA JUNI 21, BAGAMOYO


Na. Andrew Chale,

MSANII nyota wa Singeli Virus Mdudu na wengine wanatarajiwa  kunogesha tamasha kubwa la Samaki Festival 2025 lenye lengo la kuinua uchumi wa Blue kupitia Sekta ya uvuvi, Bagamoyo Mkoa wa Pwani linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ya Juni 21, 2025 eneo la Old Boma.

Kwa mujibu wa Clara Premsingh, Mkurugenzi wa Creators Hub, akizungumza kuhusu Samaki Festival 2025 amesema wazo la tamasha hilo ni kuleta burudani, biashara pamoja na Utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa Blue.

Clara amesema Wasanii wa Singeli na vikundi mbalimbali vya burudani vitakavyopiga muziki wa 'live' watachangamsha tamasha hilo.

Msanii wa Singeli, Virus Mdudu 


"Wakazi wote mnakaribishwa hakuna kiingilio.

Wasanii nyota wa Singeli kama Virus Mdudu pamoja na wengine watakuwepo.

Amewataja baadhi ya Wasanii wengine kuwa ni: Timitee, The Birds, Dartone Mnyama, Welle, Micky Singer, Safari  Rockers ambapo hao watapiga muziki wa moja kwa moja wa bendi "Live Band,"

na Wasanii wengine ni Dogo Zero na wenzake ambao wao watapiga singeli (playback).

Aidha, amesema Samaki Festival ni la kipekee na Wana Bagamoyo na viunga vyake pamoja na majirani zake Dar Es Salaam watafurahia tamasha hilo.

"Wavuvi watapewa elimu  sahihi ya biashara kupitia Sekta ya uvuvi,

Lakini pia bidhaa za bahari ikiwemo Samaki wa kila aina watauzwa kupitia tamasha hili.

Mje muone bidhaa za Samaki "sea food" na nyingine, Samaki, pweza na wengine watauzwa na vyakula mbali mbali.

Clara amesisitiza kuwa, wadau watafurahia tamasha hilo kwani pia Ulinzi umeinarishwa wa kutosha kutoka kwa Jeshi la Polisi Bagamoyo na kampuni ya SGA.

Tamasha ambalo linatarajia kufanyika katika jengo la Mjerumani "Old Boma" , asubuhi hiyo ya Juni 21 kutatanguliwa na michezo mbalimbali ikiwemo Jogging, mpira wa miguu wa ufukweni, lakini pia kutakuwa na safari za Kitalii ndani ya boat ambayo itawazungusha wageni kwenda kwenye kisiwa kilichopo eneo hilo la Bagamoyo, pamoja na Utalii mwingine ambao watatembelea maeneo ya kihistoria ya mji huo wa kale pamoja na shamrashamra zingine.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI