Header Ads Widget

MAMLAKA YA MELI NCHINI (MSCL) WATAKIWA KUWA WABUNIFU





Na chausiku said ,MDTV Mwanza.

Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete ameitaka mamlaka ya meli nchini (MSCL) kuwa wabunifu katika kutafuta masoko yatakayoweza kusaidia kuongeza kipato cha Taifa kutokana na meli mpya inayojengwa ya Mv Mwanza hapa kazi tu.

Mwakibete ameeleza hayo wakati akifanya ziara yake Mkoani Mwanza ya kukagua miradi ambayo inasimamiwa na kampuni ya meli nchini.

Ameeleza kuwa mradi huo wa ujenzi wa meli mpya ya kisasa ambao utagharimu sh Bil. 97 na tayari sh Bil. 77 imeishatolewa kwa mkandarasi ili aweze kuendelea na kazi ya ujenzi wa meli hiyo.

Mwakibete amesema kuwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo mkubwa wa kubeba abilia 1200, mizigo tani 400 na uwezo wa kubeba magari madogo 20 na magari ya kati 3 itasaidia kwa kiwago kikubwa kuongeza pato.

"Tunategemea meli hiyo iwe inafanya kazi kutoka mwanza na kwenda kagera pamoja na visiwa vya uganda, hivyo wafanye utafiti wa masoko hususani nchi jirani ya kenya mji wa kisumu" alisema mwakibete.

Amefafanua kuwa meli hiyo inapaswa kufanya kazi katika nchi za mashariki ili kuweza kuteka soko la kibiashara kutokana na meli hiyo kuwa ya kisasa na bora ambavyo haijawahi kutokea.

Mwakibete ameleeza kuwa kutokana na changamoto ya Covid 19 ilipelekea meli hiyo kutokamilika kwa wakati kama ilivyopangwa awali na kuwataka wakandarasi ifikapo mwezi 9 mwaka huu meli hiyo kukamilika kama ambavyo mkataba wao unaeleza na kama watashindwa kukamilisha itawabidi kuilipa serikali.

Kwa upande mwingine ameweza kukagua meli ya kubeba mabehewa Mv Umoja na kueleza kuwa ni meli ambayo ni kuongo muhimu kwa wafanyabiashara wote nchini hususani wanaotoka nchini uganda.

Mwakibete amempongeza Rais Samia kwa kutoa sh Trion 14.4 kwa ajili ya kurekebisha reli ya SGR ambapo ameeleza kuwa uwepo wa reli hiyo utasaidia meli hizo kufanya vizuri katika upande wa kupeleka biashara nchi jirani ikiwemo uganda.

"Ikumbukwe 2% ya bidhaa zote zinapita bandari ya dar-es salam ndizo zinazokwenda uganda" Alisema Mwakibete

Aidha ameeleza kuwa malengo ya wizara ni kuona angalau wanafikia 40% kuhakikisha wanateka soko lote la uganda na kwa sasa Tanzania inafanya vizBil. hususani katika  biasahara za mizigo inayopita nchi nyingi 36% ya biashara zinakwenda kongo,  26% zambia.

Mwakibete ameeleza kuwa sehemu ambazo Tanzania haifanyi vizuri kibiashara ni pamoja na uganda ambapo ni 2% Burudi 5% Rwanda 7% na Malawi 7%

Ameeleza kuwa wanahitaji kuwekeza nguvu zaidi upande wa uganda na kenya kuhakikisha wanakuza soko la kibiashara.

Kaimu Afisa mtendaji Mkuu wa huduma za Meli Mkoani Mwanza Philemon Bagambilana ameeleza kuwa serikali awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu imewekeza sana katika sekta ya uchukuzi na kipekee katika usafiri wa njia ya maji.

Philemon amesema kuwa Taasisi hiyo ya huduma za meli imezidi kufanya utekewezaji mkubwa itakayokamilika na kuleta ushindani wa soko katika nchi za Afrika nzima.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI