.
Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.
Viongozi wa dini ya kikiristo jimbo la Bukoba mkoni Kagera wameombwa kufikilia kujenga sehemu ya makumbusho ya jimbo hilo ili kutunza historia ya jimbo hilo.
Kauli hiyo imetolewa na makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango katika kanisa kuu la Cathederal lililopo halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani kagera katika maadhimisho ya miaka 50 ya upadre wa askofu wa jimbo katoliki la Bukoba mhashamu askofu Method Kilaini akimuwakilisha rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan.
“Nafahamu baba askofu Method Kilaini umeandika kitabu kinachoelezea historia ya jimbo hili na nafasi yake katika kueneza injili nakupongeza sana, lakini sasa ninaombi kwa viongonzi wa jimbo hili kufikilia kujenga makumbusho makubwa yanayoendana na ukubwa na historia ya jimbo hili na kupitia makumbusho hayo waamini pamoja na wananchi wa mkoa huu watapata fursa ya kipekee ya kuijua histolia ya kanisa, mkoa huu wa kagera na mchango wake katika taifa la Tanzania kwa undani zaidi”
Aidha, Dkt. Mpango amempongeza mhashamu askofu Method Kilaini kwa kufikisha miaka 50 ya upadre kwani serikali inatambua mchango wake mkubwa katika nchi hii hasa katika kuubiri amani katika nchi hii.
Sambamba na hilo Dkt.Mpango amewaomba viongozi wa dini kutilia mkazo katika mahubiri yao juu ya umuhimu wa kulinda na kudumisha amani ya nchi hii.
Kwa upande wake mhashamu askofu wa Jimbo la Bukoba Method Kilaini ambaye alikuwa anaadhimisha miaka 50 tangu alipopata daraja la upadre amemshukurumwenyezi Mungu kumuwezesha kuyashinda mambo yote ambayo amekuwa akikumbana nayo na kumuwezesha kufanya kufanya kazi ya kueneza neno lake, Mkamu wa rais viongozi wa serikali, viongozi wa madhehebu yote pamoja waumini kwa kuungana naye katika siku hii muhimu kwake na kuahidi kuwa ataendelea kueneza neno la Mungu mpaka utakapofika ukomo wa maisha yake.
“Ninapoadhimisha jubilei yangu ya dhahabu namshukusu mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye aliyeniwezesha, ndugu zangu upadre si lele mama ninapoadhimisha miaka 50 ya upadre nawaambia upadre sio lelemama kuna milima na mabonde, kuna kalaa na raha, Kuna wakati wa uzuni na furaha yote haya nimepitia na napenda kuwaambia hata siku moja sitajutia kuwa padre nimepitia mengi lakini nimevuka”
0 Comments