Header Ads Widget

KAMA MMESHINDWA SIASA TAFUTENI KAZI ZINGINE" MABODI

 



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Mabodi amewashauri wanasiasa ambao wameshindwa kazi za kisiasa watafute kazi zingine za kujiingizia kipato na kwamba wananchi hawahitaji siasa za kuuza maneno na porojo bali wanahitaji maendeleo endelevu.


Dkt. Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,ameyasema hayo kwenye kongamano lililoandaliwa na UWT na kufanyika  Amani Mkoa Zanzibar ili kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani.


Amewaonya baadhi ya Wanasiasa kuacha tabia za kutafuta ‘Kiki’ za kisiasa kwa kuwachafua viongozi wa Serikali na Chama badala ya kusifia maendeleo yaliyofikiwa nchini. Dkt.Mabodi amesema genge hilo la wanasiasa limekuwa likitangatanga kila kona likibeza na kupotosha juhudi na hatua kubwa zinazofanywa na Serikali zote mbili.


Kiongozi huyo amewambia wanasiasa hao wanaotoka katika moja ya Chama cha Upinzania Zanzibar kuwa waache mtindo huo wa siasa chafu bali wajipange kushindana kwa Sera za maendeleo yaani waonyeshe mambo waliyoyatekeleza kwa wananchi kama inavyofanya CCM.


"Tunayo mengi ya kujivunia na kutamba sasa na nyie wenzetu semeni yenu mliyowafanyia wananchi ?,,.sio mnasubiri sisi tufanye eti nyie muanze kupotosha na kukosoa twambieni Unguja na Pemba wapi mmejenga shule,hospitali,visima vya maji safi na salama hata msaada mdogo tu wa kijamii kwani ruzuku mnapata.”  Alihoji Dkt.Mabodi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI