Header Ads Widget

VIJANA WANATISHWA NA WAZAZI KUOMBA MIKOPO

IMEELEZWA   kuwa  kutokana na  uelewa  mdogo  na  hofu ya  baadhi ya  wazazi juu ya  mikopo mbali  mbali  inayotolewa na Halmashauri  na taasisi  nyingine  za  kifedha  imepelekea kurudisha  nyuma maendeleo  ya  baadhi ya  vijana  katika  wilaya ya Mufindi  mkoani Iringa  ambao  wamekuwa  wakizuiwa  na  wazazi  wao kujitokeza  kuomnba mikopo .

Haya  yamebainika   Leo wakati wa  warsha ya  siku  10 ya   ujasiriamali kwa  vijana  100   wanaotoka  katika mazingira  magumu  kata  za  Ihanu ,  Mdabulo  na  Luhunga  wilaya  ya  Mufindi  ,  walisema   baadhi ya  wazazi  wamekuwa  wakiwazuia   kujiunga  vikundi  vya  vijana   ili  kuomba mikopo  mbali mbali  itakayowezesha   wao kupiga hatua  katika uanzishaji  wa  miradi ya  kiuchumi .


 Anles Msindila kutoka  kijiji  cha Iyegeya   alisema  kuna haja ya mafunzo  ya  elimu  juu ya ujasiriamali  na  faida ya  kuchangamkia  fursa  mbali mbali  zinapotangazwa   kuendelea  kutolewa  kwa  vijana  pamoja na  wazazi  ili  kuondokana na masikitiko ya  ugumu  wa maisha  huku  fursa  zinapotangazwa  za  mikopo zikiendelea  kuwapita  kushoto  kutokana na hofu ya  baadhi ya  wazazi.

" Vijana  baadhi  hatukuwa na  elimu  ya  kutosha  juu ya  uibuaji  wa  fursa na jinsi ya kuzitumia   fursa  husika na  jinsi ya kufikiwa na mikopo  mbali mbali lakini kupitia mradi  huu  wa Youth Agence  Mufindi (YAM)  tumeweza  kubaini  fursa  mbali  mbali  ambazo  tunaweza  kwenda  kuziibua na  kuzitumia  ili  kuondokana na changamoto  ya hali  duni ya maisha " alisema 


Alisema  kuwa  wao kama  vijana  wanatamani kuchangamkia   fursa  ya mikopo  ambayo  serikali  imekuwa  ikitangaza  lakini  wamekuwa  wakiwakatisha  tamaa  kwa  hofu  ya  mikopo   hiyo  kutorejeshwa na kuingia kwenye  matatizo  ya  kuchukuliwa  hatua ya  kushindwa  kurejesha  mikopo .

Hata  hivyo  alisema  kutokana na  mafunzo  hayo  kwa  sasa anaamini kabisa  atakwenda  kuwa  chachu  kwa  wenzake  kwa  kuchangamkia  mikopo  na  fursa  nyingine  ili  kubadili mwelekeo  wa  maisha yake  kiuchumi .

Pia  aliomba   serikali  kuendelea  kutoa  mikopo  kwa   vijana  pamoja na   elimu  juu ya  usahihi ya  kuendesha  miradi  na  jinsi ya  kurejesha  mikopo   husika.

 Kwa  upande  wao  wajumbe  wa kamati  za ulinzi  kwa  watoto  na vijana  vijijini (VCPC) Anold Kinayevene  na  Augustino Julius  walisema  kuwa  kumekuwepo na mabadiliko  makubwa ya  mwenendo  wa  kimaisha  na  kiuchumi  kwa   vijana  ambao  wapo  kwenye  mradi  huo  tofauti na awali kabla ya  mradi  kuanza .

Kuwa   vijana hao  wana Fursa kubwa  za  kufanya katika vijijini   vyao  zikiwemo  za  ufugaji  wa  nguruwe ,kuku  na mifugo  mingine kikiwemo  kilimo  cha  mahindi  mabichi  (gobo)  pamoja na  changamoto  ya  kuzuia  wanyama  waharibifu kama ngedere .


Hivi  karibuni  akizungumza na  vijana  hao mkuu  wa  wilaya  ya  Mufindi Saad  Mtambule mbali ya kuwapongeza  waratibu  wa  mradi  huo  bado  aliwataka   vijana  ambao  wamebahatika  kuingizwa kwenye  mradi  kwenda  kuwa  wabunifu  wa   miradi  vijijini kwao na  kuwataka   vijana  kupitia mradi  huo kuunda vikundi vya kiuchumi ili kunufaika na mikopo isiyo na riba toka Halmashauri badala ya kukaa Vijiweni bila kazi .



Alisema serikali ya wilaya haitapenda kuona vijana wakizurula mtaani ama kushinda Vijiweni bila kazi na kuwa watakaokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wafungwe gerezani wakafundishwe kufanya kazi huko.


Aliongeza kuwa baada ya kupata mafunzo hayo jambo la msingi ni kuyatekeleza kwani utekelezaji wao utapunguza mazingira ya vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia katika jamii zao  huku akiwataka kuwatumia viongozi wao wakati wanapohitaji msaada



Meneja wa mradi wa YAM Zilpa Mgeni alisema   mradi huo unaendeshwa Kwa ushirikiano  na serikali na hivyo wanaishukuru  serikali kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na mradi wao ambao kiujumla una msaada mkubwa sana kwa vijana 

''Mimi na timu yangu tumeona huu mradi unasaidia kwasababu tumegundua kuwa kuna mbadaliko makubwa tangu tumeanza kuwabainikwani hapo mwanzo walikuwa hawajiaamini kwamba wanaweza kufanya biasharalakini baada ya kupata mafunzo ya saikolojia na ujasiriamali wao wenyewe wamekiri  kwamba wanaweza kufanya kitu ''. alisema  Zilpa


Pia aliiomba serikali kuzidi kutoa ushirikiano hasa kwa kusaidia kupatikana kwa mikopo hiyo ili wanufaika hao wapate mitaji na kuweza kujiendeleza kimaendeleo.

Akizungumzi faida ya mafunzo  haya meneja  wa mradi  wa Youth Agency Mufindi (YAM) Zilipa alisema lengo la mafunzo hayo ni   kuwawezesha  vijana  zaidi ya  770 wakiwemo  watoto  150 yatima  kutoka   kata   hizo tatu   ambazo  zote  zitaunganishwa na  vijiji  16  za  mradi  huo .


Alisema  mradi  huo wa  YAM ni wa miaka minne toka mwaka 2021/2024 umefadhiliwa na    serikali  ya Filands  chini ya taasisi yake ya Diaconess   kwa  ushirikiano  wa  serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya  wilaya  ya Mufindi na taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation.(FCWC)                                                                                                                                               Mgeni  alisema  baada ya mafunzo hayo  kutolewa kwa  walengwa  watawezeshwa  mitaji ya  kuendeshea miradi  ambayo watakuwa wamechangua  kuifanya kwa  kuwaongezea  nguvu ya  kuiboresha  zaidi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na diwani wa kata ya Luhunga Festo  Mgina aliwataka vijana hao  kusikiliza vyema mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwa pamoja na kuwahakikishia kupata mikopo baada ya mafunzo  yao kutokana na serikali kujipanga vyema katika kuwasaidia wahitaji.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI