Header Ads Widget

DR. KIJAJI ATOA MAAGIZO KWA TUME YA USHINDANI (FCC)

Waziri wa uwekezaji viwanda na Biashara Dkt,  Ashatu kijaji ameitaka tume ya ushindani (FCC) nchini kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wanaboresha mifumo ya kifedha ili kuhakikisha athari zinazoweza kutokea haziwaathiri watumiaji MWANDISHI CHAUSIKU SAID MDTV MWANZA

Dkt, kijaji ameeleza hayo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya haki ya mtumiaji Duniani yaliyofanyika jijini hapa na kusema  kuwa tume hiyo ni lazima kufanya tathimini katika masoko ili kuweza kubaini mapungufu yaliyopo katika kumlinda mtumiaji wa huduma za kifedha.

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa kufanya tathmini ya matokeo ya utafiti husika na kuishauri Serikali kuhusiana na mahitaji mapya ya Kisera, Taratibu na Kanuni kuhakikisha kuwa Jukumu la Msingi la Kumlinda Mtumiaji wa Tanzania, hususani katika Sekta zisizo chini ya Mamlaka za Udhibiti wa Kisekta zinaboreshwa.

"Ninafahamu kuwa kwa sasa kuna jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa huduma za Kifedha Kidigitali zinatolewa kwa kuzingatia haki, usawa na usalama kwa watoa huduma na wateja kama vile uwepo wa Baraza la Kitaifa la Kusimamia Mfumo wa Ushirikishwaji wa Wananchi katika Huduma za Kifedha pamoja na Sheria, Taratibu na Kanuni mbalimbali zinasimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta ya Mawasiliano (TCRA) pamoja na Benki Kuu ya Tanzania.

Dkt, Kijaji ameeleza kuwa  licha ya jitihada hizo, bado Mfumo wa Usimamizi na Udhibiti wa Huduma za Fedha Kidijitali ni eneo jipya katika uchumi linalohitaji msukumo mkubwa wa kipekee wa mbinu na teknolojia za kisasa za Udhibiti na Usimamizi ili kuhakikisha kuwa Watumiaji wa Huduma za fedha Kidijitali wanalindwa, sambamba na Kaulimbiu ya maadhimisho ya haki za Mtumiaji kwa Mwaka huu.

Ameeleza kuwa ni lazima  kubaini maeneo ya maboresho katika kuiongezea nguvu na mawanda Sheria ya Ushindani, 2003 ili kuiwezesha mamlaka ya utekelezaji sheria katika kushughulikia na kutatua malalamiko ya watumiaji wa huduma za kifedha na maeneo mengine mahususi ya kumlinda mtumiaji. 

"Sisi kama Tanzania sio kisiwa, tunaishi na Mataifa mengine Duniani ambapo kwa kiasi kikubwa tunaunganishwa na mifumo ya kidigitali, ikiwemo  mifumo ya kifedha,  Utafiti uliofanywa Mwaka 2020 na Taasisi ya Juniper, umebainisha kuwa mpaka kufikia Mwaka 2024 inakadiriwa kuwa watu zaidi ya bilioni 3.6 ambao ni 50% ya watu wote duniani watakuwa wakitumia huduma za kibenki za kidjitali" alisema Dkt, kijaji. 

Ameeleza kuwa kwa kutambua changamoto zinazoambatana na mifumo ya fedha kidigitali, kama vile tatizo la usalama hafifu wa kimtandao ipo haja ya kuliangalia eneo hilo kwa umakini  ili kuhakikisha Mtumiaji wa Huduma za Fedha Kidijitali analindwa dhidi ya athari hasi na changamoto zinazoweza kujitokeza sokoni katika miamala na huduma zinazohusisha matumizi ya fedha kidijitali. 

Hata hivyo amefafanua kuwa jitihada hizo, bado Mfumo wa Usimamizi na Udhibiti wa Huduma za Fedha Kidijitali ni eneo jipya katika uchumi wetu linalohitaji msukumo mkubwa wa kipekee wa mbinu na teknolojia za kisasa za Udhibiti na Usimamizi ili kuhakikisha kuwa Watumiaji wa Huduma za fedha Kidijitali wanalindwa.


Aidha ameeleza kuwa ni muhimu kwa Tume ya Ushindani kushirikiana na Taasisi zote zinazohusika na udhibiti ili Serikali iwe na suluhisho la pamoja katika eneo hili la kumlinda mtumiaji. 

"Ushirikiano ninaozungumza hapa ni ule wa kiuwezeshaji na siyo mwingiliano wa masuala mahususi ya kiudhibiti, Aidha ni muhimu ushirikiano huo uzingatie Mbinu Bora za Utendaji Kimataifa" alisema kijaji.

Mwenyekiti wa tume ya ushindani Aggrey Mhimuka ameeleza kuwa tume hiyo inazamana ya kushughulikia maswala ya kumlinda mtumiaji

"Katika nchi zilizoendelea ikiwemo marekani,  Australia na nchi zingine za ulaya maswala ya utekelezaji sheria za ushindani na sherilia ya kumlinda ntumiaji zinafanyika kwa ufasaha"alisema Mhimuka

Aidha amefafanua kuwa kwa mjibu wa Mfuko huo msingi wa kushughulikia maswala ya mtumiaji wa fedha unaongozwa na nguzo tatu,  moja ni kuhusu elimu ya fedha hii inalenga kwa watumiaji wa fedha kufahamu haki na wajibu wao.

Hatua nyingine ameeleza kuwa ni namna ya kufahamu aina mbalimbali za huduma za kifedha na kupata maarifa namna ya kutunza rasmali fedha zao na misingi ya kumlinda mtumiaji wa fedha pamoja na kufahamu taratibu za kutatua kero na malalamiko na kuweka ufatiliaji

usimamizi na uthibiti wa vitendo vinavyokiuka misingi anayotumia mtumiaji.

Ameeleza kiwa ulimwengu wa sasa unatawaliwa na jamii iliyounganishwa na miundombinu na shughuli za uwekezaji kwa kitumia mitandao ya kijamii hususani upatikanaji wa fedha kidigitali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa (FCTp) Jaji Salma Maghimbi ameeleza kuwa utelezaji wa kisheria ni fursa muhimu inayoweza kuwasaidia kujifunza kuhusu kanuni na mbinu za kurudisha maishauri ya ishindani na kumlinda mlaji ili aweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uwasilishaji wa mashauri.

Jaji maghimbi amesema kuwa Baraza linatambua ulimwengu wa sasa umelaisisha na kuunganisha masoko kwa wanunuzi na wawekezaji kwa kutumia teknolojia mbalimbali zinazowezesha utendaji wa kibiashara kwa mtandao ikiwemo huduma ya kifedha kidigitali.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI