Header Ads Widget

WAKEREWE NA UDUGU WA DAMU II

 


Adeladius Makwega

DODOMA.


Maandishi ya E.S Gesase katika maandiko yako ya utamaduni anasema kuwa Wajita waliokuwa Majita walikuwa wakipita Ukerewe na kwenda kutafuta vyuma huko Uzinza huku Wakerewe wakiwasumbua mno.


“Mgogoro huo ulisababisha Chifu wa Wajita anayefahamika kama Kusaga na Chifu wa Wakerewe Machunde kujenga udugu baina yao na kuondoa tofauti zao. Jambo hilo la kukubaliana kuondoa ugomvi lilikuwa jepesi kwa sababu moja kubwa kuwa Ukerewe yenyewe kulikuwa na ugomvi wa ndugu kwa ndugu uchifuni. Yaani Chifu Machunde na kaka yake alikuwa anafahamika kama Machumu.” 


Machumu alitaka kumpindua kaka yake Machunde ili yeye awe chifu, kwa usalama Chifu Machunde alikubaliana kupatana na Wajita ili awe marafiki wa kumlinda pale anapopata tatizo.


“Machumu aliendelea na nia hiyo aliposhindwa mapinduzi yake alikimbilia kwa Wajita ili kuwa salama kwa Chifu Kusaga. Chifu Machunde alimuomba Chifu wa Wajita kumrudisha Machumu kwao na kweli Chifu Kusaga alifanya hivyo kwa kuwa walikuwa wamepatana. Machumu alikabidhiwa huko, huku macho yake yakiwa yameondolewa na jambo hilo lilikuwa ni kumpunguza nguvu na kuondoa vurugu akirudi Ukerewe.” 


Jambo hio lilijenga udugu mkubwa kwa Wajita na Wakerewe wakawekeana nadhiri wakaondoa uadui na wakawa watani hadi leo hii.


Mtafiti C M K. Magogo anakwenda mbali kwa kusema kuwa Machumu alitobolewa macho kwa hoja moja kubwa kuwa kipofu kwao ilikuwa haruhusiwi kupewa majumu yoyote ya uongozi.

KIbaya zaidi wale waliokuwa machifu wa Wakerewe walikuwa na tabia ambazo ziliwauzi wengi ikiwamo na tabia ya kuoa kwa lazima wanawake waliokuwa wakionekana warembo bila ya kujali kama hawa ni ndugu zao. Jambo hilo lilikuwa baya sana na lilileta migogoro mikubwa baina yao.


Katika kabila hili kulikuwa na makundi matatu la watu kwanza Abahango kundi hili bila ya kujali ni masikini au tajiri hawa walitakiwa kuheshimiwa mno, hili ni kundi la watawala. Kundi lingine ni wale masikini ambao hawa ni watu duni kabisa hawakuruhusiwa kuoa kwa akina Abahanga, bali akina Abahanga walirusiwa kuoa mwanamke yoyote mrembo wa kundi hili.


Ilikuwa ikiaminika kuwa kwa Wakerewe wanawake wazuri walikuwa wakizaliwa nje ya familia za machufu. Kati ya machifu 17 wa Wakerewe machifu 15 walio kutoka tabaka la masikini bali machifu wawili tu ndiyo walioa kwa machifu wenzao.


Ndoa hizo nyingi zilikuwa za kulazimisha si hiari. Kabla ya ndoa hiyo ilitakiwa kutolewa kitu kama fidia kule anapotokea binti huyo nayeolewa kupewa fahari(Ng’ombe dume mkubwa) na ile familia ya chifu.


Wakati wakikabidhiwa dume hilo la ng’ombe waliambia wanaweza kupokonywa muda wowote ule dume hilo linapohitajika na chifu, huku binti yao akichukuliwa kwa nguvu.


Kulingana C S K Magogo anasema kuwa Ukoo wa Abahemba na Abaluhu wana mahusiano na Abasita na Abayango na Abatundu lakini Abasilanga wana udugu na Abasita kwa sababu ya kiongozi wao alikuwa Bunini. 


Bunini na Luhinda wote walikuwa watoto wa Nkombya ambapo ilidaiwa kabla ya kufa huko Bukoba aliacha wosia kwa watoto wake waondoke Bukoba wasiishi hapo tena


Wabahilla na Wabazigaba hawa wote ikiaminika kuwa alifika Ukerewe wakitokea Musoma kwa Wajita. Wabahila walifika wa kwanza, Watu waliowakuta walipigwa na kuwafurusha na wakaanza kuishi wao katika eneo ambalo lilifahamika kama Bwiru (Kijiji Changu) lakini baadaye Abazigaha wakavamia  kisiwa kizima cha ukerewe.


Wabazigaba na Wabahila walikuwa ndugu kabla ya kutokea huko Bukoba na walipofika Ukerewe japokuwa walikuwa mtu na mdogo wake na walianza kuoleana na hapo ukaibuka utani baina yao.


makwadeladius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI