Header Ads Widget

WAKAZI WA RUVUMA WATAKIWA KUTUMIA MIFUKO ILIYOELEKEZWA NA SERIKALI.

 


 


NA AMON MTEGA, RUVUMA .


WAKAZI  wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kutumia mifuko ya plastiki (Vifungashio)iliyoelekezwa na Serikali ili kulinda Mazingira pamoja na Afya za watumiaji wanaonunua bidhaa(Vyakula)sokoni  na kuweka kwenye mifuko hiyo ambayo mingine haina  ubora.



Wito huo umetolewa na Meneja wa Mazingira kanda ya kusini (NEMC)Mhandisi Boniphace Guni wakati akipita kutoa elimu juu ya matumizi ya mifuko hiyo pamoja na kukagua maduka ambayo yamekuwa yakijihusisha kuuza mifuko isiyo takiwa.




Meneja Guni akitoa elimu ya matumizi ya mifuko hiyo  kwa baadhi ya  wakazi wa Manispaa ya Songea Mkoani humo pamoja na wauzaji wa mifuko hiyo waliopo kwenye Soko kuu la Songea Mazese na maeneo mbalimbali mkoani humo  amesema kuwa zoezi hilo limefikiwa kufuatia kanuni za usimamizi wa mazingira za kupiga marufuku mifuko ya plastiki za mwaka 2019 sheria ya usimamizi wa mazingira sura ya 191.





 Guni amesema kuwa kumekuwepo na mifuko ambayo haitakiwi kwa mjibu wa sheria  lakini bado baadhi ya watu wanaendelea kuitumia jambo ambalo hupelekea  uharibifu wa mazingira pamoja na Afya za binadamu kutokana mifuko hiyo kutokuwa kwenye ubora unaotakiwa.




 Amesema kuwa elimu hiyo inapita kutolewa katika maeneo yote ya mkoa wa Ruvuma na kuwa mifuko hiyo  inatakiwa kutumika ni ile yenye alama zote tano  baadhi ambazo ni nembo ya TBS sehemu ya  kiwanda husika kilipo ,uwezo wa mifuko  hiyo.




Naye mwenyekiti wa Soko kuu la Songea Mohamed Ngoyanga amesema kuwa atapita kutoa elimu ya matumizi ya mifuko hiyo ili kila mfanyabiashara (Mjasiliamali )aweze kuwa na uelewa sahihi juu ya mifuko hiyo .


 Kwa upande wake George Mgaya ambaye ni mmoja kati ya wenye maduka yaliyokutwa na mifuko ambayo haistahili  amesema kuwa elimu hiyo itawasaidia kuwa waangalifu pindi wanapochukuwa bidhaa ya mifuko hiyo.



Hata hivyo Afisa Mazingira wa Mkoa wa Ruvuma Sarah Mokeha amesema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu katika mkoa huo ili kila mwananchi aweze kuwa na uelewa wa umuhimu wa kutunza mazingira kwa kutokutumia mifuko isiyofaa .




Katika utoaji wa elimu hiyo iliambatana na kuyakagua maduka yanayouza mifuko na baadhi ya maduka yamekutwa na mifuko ambayo imekatazwa na Serikali na kuwa wamechukuliwa hatua ya kulipa faini kwa baadhi yao kwa viwango mbalimbali.


        

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI