Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA BIMA.

 



MWANZA.



Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza wapatiwa mafunzo ya bima ili kupata uelewa juu ya jambo hilo na kuwa mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii.



Naibu kamishna wa mamlaka ya bima Taifa Khadija Issa ameeleza kuwa lengo la kuwajengea uwezo wakati wanaandika habari mbalimbali kuhusiana na bima na kujipambanua na kuwa waandishi wa habari za bima.




Ameeleza kuwa waandishi wa habari ndio wanauwezo wa kutoa elimu katika ngazi zote za jamii na watu kupata uelewa juu ya bima .



"Tunajua mnaweza kuwafikia kila kona nankila pembe ya nchi hii kwa hiyo tunawategemea sana kuwafikia wananchi wetu popote walipo" Alisema khadija.



Khadija ameeleza kuwa zaidi ya asilimia 75 ya watanzania wanamiliki simu za mkononi na waandishi wa habari wanaweza kuwafikia kwa kutumia simu zao, Radio, Televisheni, Magazeti na Mitandao ya kijamii.



"Tukiamua kila siku kila chombo cha habari kikitoa taarifa moja tu ya bima basi angalau asilimia 75 ya watanzania watakuwa wamefikiwa na elimu ya bima kuweza kuwasaidia na kuwaokoa wananchi kutoka kwenye majanga mbalimbali kama vile moto, ajali na madhara" Alisema Khadija.



Ameeleza kuwa bima ina umuhimu kubwa katika ngazi zote za familia hadi Taifa kutokana na ustawi pamoja na kupata huduma mbalimbali.



Khadija ameeleza kuwa maswala ya bima bado hayapewi kipaumbele katika jamii, uelewa wa bima bado ni mdogo kwa watanzania kuna changamoto katika kuzifikia huduma za bima.



" Ni imani yetu wanahabari mkiamua mnaweza kuikuza sekta ya bima na kuwaokoa wananchi wetu dhidi ya majanga mbalimbali"Aliema Khadija.



Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya bima kanda ya ziwa (TIRA)Sharif Ali Hamadi ameeleza kuwa kuwajengea waandishi uelewa itakuwa rahisi kufikisha ujumbe kwenye jamii kuhusu bima.



Sharif ameeleza kuwa wamepewa jukumu la kusimamia maswala ya bima katika nchi yetu na baadhi ya majukumu yanayofanywa na bima ikiwa ni pamoja na kusimamia upatikanaji wa bima, kushughulikia malalamiko yote ya bima kutoka kwa watumiaji.



"Kama mnavyoelewa majanga ya moto yamekuwa mengi sana majumbani lakini pia mashuleni pamoja na viwandani na kusababisha kupoteza maisha ya watu na mali zao.



Edwini soko mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) ameeza kuwa swala la bima kwa waandishi linanafasi kubwa hususani bima ya Afya wanapokuwa kwenye majukumu.



Soko ameeleza kuwa Waandishi wa habari sio daraja na wao pia wanahitaji kunufaika katika bima hizo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI