Teddy Kilanga _Arusha
Wanawake wafanyabiashara mipakani katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki wameomba serikali za nchi wanachama kuhimarisha sera zitakazolinda katika shughuli zao.
Awali akizungumza februari 24,2022 katika kikao cha mjadaliano ya pamoja na wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki,Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania,(TAMWA) Dkt. Rose Ruben amesema kwenye maeneo ya mipakani wanawake wanakabiliwa na changamoto ya kubuguziwa katika biashara zao.
Dkt.Ruben amesema wanawake wanapata changamoto ya kubuguziwa katika maeneo yao ya biashara kwenye mipaka ya nchi za EAC hali iliyopelekea kujadili nakuona ni namna gani wataziondoa changamoto hizo.
"Tumeona wanawake wengi katika maeneo ya mipaka wanapofanya biashara hawana imani ya kuweza kukaa kutokana na kutojuana lakinj pia hawafahamu sheria na taratibu zinazofanyika ili waweze kufanya biashara zao vizuri,"amesema Dkt.Ruben.
Aidha amesema linapotokea jambo la namna hiyo ni lazima watokee wadau wanaoweza kuliibua ili wenye mamlaka ya kuweza kutengeneza sera na kutunga sheria ambayo itakuwa njia ya kusaidia wanawake wafanyabiashara wanaoathirika na biashara za mipakani.
Pia amesema ni vyema wakajitokeza wadau wa kusaidia kuelimisha wanawake hao kuhusiana na umuhimu wa kuweza kuzirasmisha ili kufahamu faida wanayoiweza kuipata katika biashara hiyo.
Naye Mkurugenzi wa mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) Lilian Lihundi amesema kutokana na changamoto hizo za mipakani ni vyema wakatekeleza sera zilizopo katika nchi wanachama katika kuhakikisha mazingira ya biashara mipakani yapo vizuri.
"Tukumbuke kwamba hawa wanawake wafanyabiashara mipakani wanazalisha ili waendeshe familia zao lakini pia ni chanzo cha pato la Taifa pale wanapozalisha hivyo ni muhimu kwa serikali kushirikiana na wanawake kuhakikisha kwamba sera zetu tulizojiwekea tunazitekeleza vizuri,"amesema Lihundi.
Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya wanawake Afrika ya mashariki(EASSI) Sheila Mishambi amesema wanapata changamoto ya kubuguziwa na wafanyabiashara wadogowadogo katika maeneo ya mipakani ambapo wanakumbana na unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukosefu wa ulinzi wa mali zao.
"Hivyo kupitia mjadala huu tunajaribu kupunguza changamoto wanazokutananazo wanawake hawa wafanyabiashara katika maeneo ya mipakani ni vyema wakaelimishwa juu ya sera na sheria zinazowalinda ili kuondoa matabaka,"amesema Mkurugenzi huyo.
Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano ya biashara na uwekezaji katika bunge la Afrika mashariki,Christophe Nauwayo amesema kutokana na wanawake wafanyabiashara kubuguziwa katika maeneo ya mipakani ni vyema wakahamasisha jambo hilo ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
0 Comments