Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI WATOA TAMKO KUHUSU HAKI NA USTAWI WA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI.

 



MWANZA, 



Kamati ya amani ya viongozi wa Dini Mkoa wa Mwanza imetoa tamko kuhusu haki na ustawi wa watu wenye ulemavu wa ngozi na kueleza kuwa jamii imekuwa ikiwachukulia kwa mtazamo hasi kutokana na kuwa na utofauti wa muonekano wa rangi ya ngozi yao na uono hafifu.



Mwenye kiti mwenza Kamati ya amani ya Mkoa ya viongozi wa dini Askofu Charles Sekelwa ameeleza kuwa Kundi hilo limejikuta katika mazingira magumu ya unyanyapaji,  vitendo vya ukatili hali ya kimaisha, kukosa elimu, kipato, na kuwa katika hatari kubwa ya maradhi ya saratani.



Sekelwa ameeleza kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakikutana mara kwa mara kwa ajili ya majadiliano na majadiliano hayo yakilenga mambo mbalimbali ikiwemo nafasi ya viongozi hao katika kutetea watu wenye ulemavu wa ngozi, kubadilishana uzoefu wa viongozi hao kuhusu huduma kwa kundi hilo.




"Sisi kama viongozi wa dini tunatambua ukubwa wa mabadiliko hasi na kushawishi mabadiliko chanya ya kifikira katika jamii juu ya haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini" Alisema sekelwa.



Hata hivyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na wadau mbalimbali ikiwemo serikali kujitahidi kuboresha na kusimamia sera zinazowalinda watu wenye ulemavu wa ngozi na sheria hizo kuwa madhubuti wanapotendewa ukatili wahusika waweze kuadhibiwa kikamilifu.



Sekelwa amesema kuwa serikali bado inapaswa kutengeneza na kusimamia sera dhabiti zitakazowapa kipaumbele watu wenye ulemavu wa ngozi hususani mama na mtoto mitaji na kutoa rasmu ya muongozo wa elimu pamoja na kuhamasisha wahudumu wa afya kuzingatia muongozo wa matibabu kutoka wizara ya afya.



Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassani Kabeke ameeleza kuwa moja ya majukumu ya kamati ya amani ya viongozi wa dini ni kitatua na kubaini mapungufu wanaanza kufanyia kazi kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa jambo hilo.




"Tukiangalia kwa sasa hali za wenzetu sio mbaya sana hata nyie mnajua tumepiga hatua lakini sio tuendelee kulala lazima tuendelee kutoa elimu na kuelimisha jamii" Alisema sheikh hassani.



Sheikh Hassani amesema kuwa kuna ulazima wa kuendelea kuwalinda kundi hilo ili waendelee kuishi kwa amani kama walivyo watu wengine wanaoishi kwenye jamii.



Nae kwa upandae wake mwenyekiti wa TAS Stalome Makoye Maliganya ameeleza kuwa poalipo na amani kuna maendeleo watu watu wenye ulemavu wa ngozi wanapokosa amani na maendeleo yao yanazidi kuwa duni.



"Tunapokosa amani familia zetu kuwa duni kiasi ambacho hatuwezi kufanya kitu chochote kile amani inaweza kufanya watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa na maisha bora na familia yenye furuha" Alisema Stalome.




Stalome ameeleza kuwa serikali kuwajengea kundi hilo uwezo na kuwapa elimu kabla ya kupatiwa mikopo .



"Wakiwapatia mikopo bila kuwapa elimu biashara zao haziwezi kuendelea na wakati wingine jamii inawatenga inakuwa ngumu kufanya biashara, mfano unapika chakula watu wanagoma kula tayari unakuwa umearibu mtaji wako" Alisema Stalome.



Aidha ameeleza kuwa wamekuwa na changamoto ya mafuta yanayowakinga ili wasiwaze kupata saratani serikali kuwekeza  katika kuwasaidia wasiweze kuungua na jua ili waweze kufanya kazi kwa kujiamini na kujenga nchi.



" changamoto hiyo ya kukosa mafuta ni kubwa hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi kutokana na kukithiri kwa jua"Alisema Stalome.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI