Header Ads Widget

DKT. KIMEI (MB) AMSHUKURU MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUWAKUMBUKA KATIKA KEKI YA TAIFA WAMEPATA MILION 250 KUENDELEZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MARANGU.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


Dkt. Charles Kimei Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro amefanya mkutano wa Wananchi Kata ya Marangu Mashariki Kijiji cha Samanga. 



Mbunge huyo ametumia mkutano huo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwakumbuka katika KEKI ya Taifa ambapo amekubali kuidhinisha Milioni 250 ili kuendeleza ujenzi wa kituo cha Afya Marangu Mashariki ambapo kituo hicho ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa kata hiyo. 


Dkt. Kimei amewataka wananchi waendelee kumuamini Rais kwani kwa muda mfupi ameweza kufanya mambo makubwa kama vile ujenzi wa madarasa, Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati, Barabara.



Mbunge huyo aliahidi kuendelea kuomba fedha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kuweza kufanikisha ukamilikaji wa Kituo cha Afya na tayari ameshatuma maombi hivyo ana matumaini makubwa Rais atamuongezea Fedha zingine. 


Pia, amewahakikishia wananchi wa Jimbo la Vunjo miradi yote inayoendelea jimboni itamalizika na wananchi watafaidika, miradi ya Maji ambayo ipo katika hatua mbalimbali na Miundombinu ya Barabara. 



Katika hatua nyingine Mbunge huyo ameahidi kuambatana na Diwani kukutana na Meneja wa TARURA ili kuweza kuona changamoto za Barabara zilizoharibika kutokana na mvua zinapata Fedha za kukarabati kupitia mfuko wa mkuu wa Serikali. 


Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Ramadhani Mahanyu amewashukuru wananchi kuendelea kukiamini na kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu Hassan, Mbunge, Diwani na Viongozi wa Serikali za Vijiji. 



Amewataka wananchi wajivunie kuwa na Mbunge kama Dkt. Kimei kwakuwa ni mchapakazi hodari na mtu wa vitendo zaidi. 


Naye Diwani wa kata ya Marangu Mashariki Jonas Mawalla amemshukuru l Mbunge Dkt. Kimei kwa kuwapambania kupata Fedha hizo Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya.  


Diwani huyo amempongeza pia Mbunge kwa kuwapambania katika miradi ya Maji, ukarabati wa madarasa ya Shule.


Pia, Mhe. Diwani ameomba wananchi wa maeneo ambayo Ujenzi unaendelea wapewe kipaumbele katika ajira za Ujenzi ili pasiwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI