Header Ads Widget

"VIONGOZI ENDELEENI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA" MHE. MARIA OMARY

 



MBUNGE wa Pandani Kaskazini Pemba na Balozi wa Mazingira pia ni mwanakamati wa uwekezaji viwanda Biashara na Mazingira Maria Omary Saidi amewaomba Viongozi kuendelea kushirikiana na wananchi bega kwa bega katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa ......,...........Hamida Ramadhan Dodoma 


Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa zoezi la Upandaji miti eneo la wazi la ISENI Dodoma jiji katika wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 ambapo kileke chake ni siku ya kesho tarehe 12 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere (NYERERE SQUARE) na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango. 


" Tunashirikiana katika kupanda miti hii hivyo nasaha zangu ni kuwaomba tuendelee katika kuitunza miti hii ili iweze kukuwa kwani Dodoma ya kijani inawezekana Dodoma ya zamani ni tufauti na ilivyo sasa hiyo yote ni kutokana na kutunza mazingira," amesema .


Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Muungano Mary Maganga amewapongeza wananchi kwani wameweza kujitokeza katika shughuli mbalimbali za usafi na upandaji wa miti na wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa.



Amesema matukio ya kupanda miti na usafi wa mazingira yasifanyike Dodoma peke yake mkoa wa Dodoma umechaguliwa kama kipaumbele hivyo wananchi nchi nzima  wawe na tabia ya kutunza mazingira na kupanda miti ili kuweza kuibadilisha nchi ya Tanzania 


Naye Kamidhina Msaidizi wa Uhifadhi wa Misitu  kanda ya kati Mathew Kiondo akiongea kwa niaba ya Kamishina wa Wakala wa uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema kupanda mti Dodoma  ni kazi rahisi sana ila kuifanya miti hiyo ikuwe ni kazi ngumu sana tuituze na tuhakikishe miti hii inakuwa.



" Kuna vitu vinavyochangia miti isikue ni pamoja na ukame na mifugo tuhakikishe miti hii baada ya mvua tuendelee kuimwagilia na mifugo haifiki katika eneo hili kwa kufanya hivi zoezi hili litakuwa endelevu kwani sio vizuri leo tumepanda miti leo na mwakani tena tunakuja kupanda katika eneo hili hili huku tutakuwa tunapoteza nguvu na pesa za serikali," amesema  


Tumepanda miti leo na tunapoitwa kuja kufanya zoezi la umwagiliaji tujitokeze kwa wingi tujitolee kuja kumwagilia maji kama tunavyofahamu kipindi cha mvua katika mkoa wa Dodoma ni kipindu cha mvua ni kifupi sana lakini kipindi cha  ukame ni kirefu pia TFS tumejipanga kutoa miche ya miti kwa kila mtu na Taasisi kwa wanaohitaji  waje kuchukua," amesema 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI