Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof, Henry Mahoo amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya GOPA CONTRACTORS kurekebisha kasoro alizobaini wakati wa zoezi la kukagua ujenzi wa tuta la Bwawa la kuhifadhi maji yanayotumika kwa shughuli za Umwagiliaji katika Skimu ya Endagaw iliyoko Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Akizungumza katika eneo hilo, Prof,
Mahoo amemuagiza Mkandarasi GOPA CONTRACTORS kuziba maeneo yanayovujisha
maji katika Bwawa hilo vinginevyo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
haitapokea mradi huo.
Aidha Prof, Mahoo ametumia muda huo kutoa
elimu ya ada na tozo za Umwagiliaji kwa Viongozi wa Skimu hiyo, baada
ya kujionea Mkulima mmoja wa kabichi pembezoni mwa Skimu hiyo akiondoa
mazao yake shambani bila kulipia gharama za Ada na Tozo za Umwagiliaji
mbele ya viongozi wa Skimu hiyo.
Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Uendelezaji Miundombinu Kimasa Ntonda, amemuagiza Mkandarasi
awasilishe mpango kazi mpya wa utekelezaji mradi huo utakaoonyesha namna
alivyojipanga kutekeleza mradi huo na kuukamilisha kwa wakati kwa
mujibu wa Mkataba ambapo pia amemshauri kazi zote zinazoweza kutekelezwa
kwa wakati mmoja zifanyike ili kufidia muda uliopotea baada ya
mkandarasi huyo kuchelewa kuanza kazi ya ujenzi wa Bwawa hilo kwa miezi
miwili.
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilisaini makubaliano na
kampuni ya Gopa Contractors ya jijini Dar es Saalam, kujenga Mfereji
mpya wenye urefu wa Mita Elfu mbili na Mianne (2,400) sanjari na
kuongeza urefu mfereji wa zamani kwa kujenga Mita Miasaba na Sabini
(770) pamoja na kuondoa tope ndani ya bwawa linalotumika kumwagilia
Skimu ya Endagaw.
Mkataba wa ujenzi wa miundombinu hiyo baina ya
Tume na Mkandarasi Gopa Contractors ni wa zaidi ya Shilingi Milioni
Miatisa Themanini.( Milioni 980) na ulisainiwa tarehe 31.08. 2021
Skimu ya Endagaw ina jumla ya Heka 230 na wanufaika Zaidi ya 100 wa kilimo cha Mahindi na Mboga mboga.
Mkulima katika Skimu ya Umwagiliaji ya Endagaw akivuna Mbogamboga aina ya Kabichi kwaajili ya kupeleka Sokoni.
Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof, Henry Mahoo akikagua Tuta la Bwawa la Umwagiliaji katika Skimu ya Endagaw iliyoko Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu Tume ya Taifa ya Bw, Kimasa Ntonda (Kulia) akitoa elimu kwa Viongozi wa Skimu ya Endagaw namna wanavyopaswa kushiriki katika ulinzi wa Miundombinu, Malighafi na vifaa vya ujenzi katika eneo hilo.
0 Comments