Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu ametoa kiasi cha shill billion 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu mbalimbali ikiwemo mabweni matano ya kulala wanafunzi wa Chuo cha maji.
Kauli hiyo, ameitoa Waziri wa Maji, Juma Aweso wakati alipofanya ziara katika chuo cha maji kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo amesema baada ya Rais Samia kusikia kilio cha changamoto za Miundombinu zilizopo katika chuoni hapo.
"Nilikuja hapa mwezi wa 12 katika mahafali ya chuo, nikaskia changamoto zenu nikazichukua nikazifikisha kwa Rais Samia, leo nimekuja na habari njema Jumatatu mtafikishiwa pesa kwa ajili ya kuanza kazi ya ukarabati"amesema Waziri Aweso.
Hata hivyo, amesema kuwa anataka chuo hicho kiingie kwenye ushindani, huku akitaka watimize malengo yao ya kua chuo bora, huku hivyo wafanye tafiti za maji zisihishie kwenye makabati Kwa kuwa sekta ya maji ina kazi kubwa.
Aidha, amemtaka Katibu Mkuu Wizara ya maji kutowapangia kazi watumishi waliofanya vibaya wizarani kwenda katika chuo hicho kwani chuo hicho sio sehemu ya maficho.
Hata hivyo, amesema lengo la chuo hicho ni kuzalisha wataalamu bora na wenye weledi wa kusimamia miradi ya maji, hivyo amesema ni lazima kila kwenye mradi wa maji kuwe na mtaalamu wa maji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho, Dr Adamu Karia ametoa mapendekezo matatu ikiwemo ukarabati wa majengo ya chuo , kuongezewa bajeti ya chuo na pamoja na kupatiwa kituo cha tafiti.
Aidha, amemuomba waziri huyo kuidhinisha chuo cha Nguludoto kilichopo Mkoani Arusha kiwe chini ya chuo hicho ili kitumike katika Tafiti zao.
Amesema kuwa, Chuo hicho kimekua na Miundombinu chakavu kutokana na chuo hicho kujengwa na kwa muda mrefu bila kufanyiwa marekebisho.
0 Comments