Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametoa tahadhari kwa viongozi wa watakaothiriki vitendo viovu vya uvuvi haramu.
Tahadhari hiyo ameitoa juni 13,2025 wakati akiendesha kika maalum cha baraza la madiwani cha kupitia ukaguzi wa hoja za mdhibiti na mkaguzi wa fedha za serikali ( CAG)
Baada ya upitiaji wa hoja hizo wakati wa kuhailisha baraza hilo amesema suala la uvuvi haramu hslikubaliki na kiongozi yoyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo ataruka nae.
Amesema vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekuwa vikitajwa kufanyika huko nyuma haviwezi kukubalika tena na yeyote atakayeshiriki atachukuliwa hatua kali.
Mtambi amesema uvuvi haramu ndio uliopelekea kuwa na uhaba wa samaki ndani ya ziwa Victoria hivyo hali hiyo haiwezi kukubariki tena.
" Nitoe tahadhari kupitia kikao hiki kwa viongozi kutojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu kwenye marneo yetu.
" Vitendo vya uvuvi haramu ndivyo ambavyo vimetufikisha hapa tulipo na hatuwezi kukubali viendelee kufanyika tena na viongozi muwe mfano wa kuigwa" amesema.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku 90 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda kuhakikisha barabara inayoelekea ofisi ya mkurugenzi kutengenezwa.
Amesema ƙutengenezwa kwa barabara hiyo kutasaidia kufikika kwa urahisi kwenye ofisi hizo kwa wananchi na viongozi katika kupata huduma mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imepata hati safi baada ya kupitiwa kwa hoja za mkaguzi wa hesabu za fedha za fedha za serikali kwenye miradi mbalimbali.
0 Comments