Header Ads Widget

CHAMWINO IKULU WAOMBWA KUCHANGIA DAMUp

 


Adeladius Makwega-DODOMA


Wakaazi wa Chamwino Ikulu wameombwa kujitokeza kuchangia damu siku ya Jumapili ya Februari 20, 2022 ambapo kituo cha Afya cha Chamwino kitakita kambi katika Parokia ya Birikra Maria Imekulata ili wakaazi hao kutoa damu ambayo inakusudiwa kuwapatia wahitaji katika kituo cha afya cha Chamwino.


Hayo yamebainishwa jumapili ya Februari 13, 2022 katika misa ya pili katika kanisa hilo ambapo hilo lilikuwa ni miongoni mwa matangazo kadhaa waliosomewa waamini hao wakati wa misa hiyo.


“Ndugu waamini ninaomba kuja kukusanya damu jumapili ijayo ili kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu wenye mahitaji ya damu katika wilaya yetu ninatanguliza shukurani zangu za dhati.”


Msomaji wa tangazo hilo aliwaambia waamini kuwa tangazo hilo linatoka kwa Mganga Kiongozi wa Kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu.


Awali msomaji wa matangazo hayo aliwaambia waamini kuwa jumapili ya Februari 27, 2022 waamini wa kanisa hilo watamuaga mmojawapo wa maketikista anayestaafu na wanatarajia kumuaga rasmi ambapo waamini hapo watamkabidhi nyumba kama zawadi yakumaliza kazi hiyo huku ujenzi wa nyumba hiyo ukikamilishwa


Kabla ya kutoa Baraka za Mwisho katika misa hiyo Padri John Mapalala alimtambulisha Frateli Aolo Robert Mabanga anayetokea Kinshansa Kongo ambaye aliwasalimu waamini hao akiwaambia kuwa amekuja Tanzania kujifunza Kiswahili.


Hali ya hewa ya eneo hili imekuwa na mawingu wakati wa asubuhi huku mchana jua kali likiwaka. Kwa juma zima mvua zimekuwa zikinyesha za kadili na wale waliojaliwa kupanda mazao mbalimbali wakiendelea kuyapalilia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI