mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,Dkt.John Pima wataalamu na watendaji na Maafisa tarafa kutekeleza wajibu wao katika usimamizi wa zoezi la anwani za makazi ili kuweza kukamilisha kwa wakati.Mwandishi Teddy Kilanga, MDTV Arusha
Akizungumza katika mafunzo ya utekelezaji wa kazi ya zoezi la anuani za makazi jijini humo, kwa wakuu wa idara ,Maafisa tarafa na watendaji wa kata wa halimashauri hiyo,Dkt.Pima alisema kupitia usimamizo mzuri wa zoezi hilo ndio njia itakayowasaidia kumaliza mapema hata kabla ya muda uliopangwa na serikali.
"Kazi kubwa ambayo itawahitaji kuisimamia ninyi ni ile ya maneno na siasa ambayo tunatakiwa kwenda kuifanya kwa weledi zaidi katika utoaji wa majina ya mitaa kwani hapo ndio kuna vurugu kubwa,"alisema Dkt.Pima.
Dkt.Pima alisema namna ya kutoa majina ya mitaa kwa mjibu wa muongozo wetu ni vikao hivyo wameweka ratiba ya njia ya kufanya ikiwa utaratibu ambao wameutoa ni kukasimisha madaraka kwa ngazi zinazofuata.
Alisema wamekasimisha madaraka katika kushusha kwa wasimamizi ngazi ya utawala ambao watakuwa wanakutana kila wiki na kuwa na ajenda mahususi inayohusu maendeleo na utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi na chini ya hapo kila mkuu wa idara atasimamia kata moja au zaidi.
Aida alisema kuwa wanatakiwa kila mkuu wa idara ahakikishe kata yake inazingatia muda ikiwa maelekezo ni kila Afisa tarafa ni lazima ahakikishe kwamba ratiba iliyotolewa inazingatiwa na ikibidi wamalize mapema kabla ya muda uliopangwa.
"Katika zoezi hilo mtendaji wa kata na diwani wanawajibu wa kuhakikisha kwamba muda uliopangwa unatekelezwa kwa kufanya kazi kwa ufanisi katika kufauta utaratibu na vigezo vyote vilivyowekwa,"alisema Dkt.Pima.
Vilevile alisema zoezi hilo lazima liwe shirikishi baina ya wataalamu ,viongozi na wananchi ili liwe rahisi kukamilika na kuondoa malalamiko yanayoweza kuchelewesha kazi hiyo na kata tano zitakazomaliza mapema zitapatiwa zawadi.
Naye Mratibu wa anuani za makazi jiji la Arusha,Doroth Absalom alisema wametengeneza mikakati ili kuhakikisha zoezi la mfumo wa anuani za makazi linakalimilika kwa wakati ambapo watatekeleza kwa kushirikiana na ngazi za kata na mitaa.
"Katika zoezi hili tutahusisha maafisa kata,watendaji wa kata,mabalozi pamoja na watu maarufu kutoka katika maeneo husika ili kurahisisha zoezi hilo liende kwa wakati na kila mmoja aweze kushiriki kikamilifu katika uwekaji wa anuani za makazi,"alisema
Pia alisema watatumia njia ya uwishwaji na uboreshaji wa zoezi liliokuwa linafanyika mwaka 2009 hadi 2012 kwa kata za mjini kati ambapo wataandika namba katika maeneo mapya na watatuamia rangi ambayo itapakwa kwenye ukuta na mageti.
Mmoja wa watendaji waliopata mafunzo hayo wa kata ya Sombetini,Maftar Robert alisema anaishukuru serikali kwa kuboresha zoezi hilo ambalo litakwenda kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu katika mitaa na kata zao.
0 Comments