Header Ads Widget

WASANII TANZANIA KIVULI JACKIE WILSON

 



Adeladius Makwega

DODOMA.


June 26 1988 ulimwengu ulishuhudia filamu mpya ya Coming to America. Katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa mwana wa mfalme wa Afrika Akeem alitakiwa kufunga ndoa na binti asiyemfahamu.


Mwana huyu wa mfalme aliamua kwenda kinyume na mila hiyo na kufunga safari hadi Amerika, kwenda kumsaka mrembo ambaye alikuwa kweli anampenda na kumuheshimu. Safari hiyo ya mwana wa mfalme ndiyo inajenga filamu yote ya Coming to America chini ya mwongozaji na mtayarishaji John Landis. 


Eddie Murphy, Arsenio Hall, Madge Sinclair na Sharl Headley waliijenga filamu hiyo ya dakika 117 tangu mwanzo mpaka tamati.


Ndani ya muda huo, mtayarishaji na mwongozaji John Landis ametumia wimbo To be loved wa mwanamuzi Jackie Wilson. Wimbo huo wenye dakika 2.29 (sekunde 149) umeonekana maneno yake yakiimbwa na muigizaji Eddie Murphy (Akeem), wakati anakutana na mpenzi wake Sharl Headley (Lisa) kwa mara ya kwanza. Akeem alirudi nyumbani kwake akishangilia kwa macho yake kumuona binti huyo mrembo, hapa Akeem ameimba kwa sekunde 48.


Mtayarishaji Landis alisonga mbele na kuutumia wimbo huu tena. Wakati Akeem alimuualika binti mrembo Lisa kucheza naye wimbo huo wakiwa wamekumbatiana.Tangu wimbo huo ukianza hadi mashairi yake yanakamilika lisa akiwa na Akeem kifuani mwake.


Hapa mtayarishaj ametumia wimbo huu To be loved wote kama ulivyo na akaongezea sekunde moja ambalo ni jambo la nadra mno kufanyika lkatika kutayarisha filamu. Uzoefu ni matumzi ya kipande kidogo cha wimbo.


To be loved ni wimbo uliobeba maudhui ya filamu hii ya mapenzi , ukiwa ni miongoni mwa nyimbo kadhaa bora duniani ambazo ziliwahi kutungwa na kuimbwa na wanamuziki Jackie Wilson wakati wa uhai wake ambaye alifariki mwaka 1984.


Cha kusikitisha mwanamuziki huyu alifariki katika mazingira magumu mno japokuwa nyimbo zake ziliweza kuongoza katika chati kadhaa za muziki na kuwaingizia vipato vikubwa makampuni kadhaa ya muziki hadi sasa.


Hata maiti yake ikizikwa katika eneo ambalo ilikuwa ngumu kutambulika lakini baadaye wapenzi wa muziki wake walichangisha fedha na kumzika eneo lenye hadhi yake. Kila mara alipokuwa akiyauliza makampuni aliyowekeana nayo mikataba walimjibu kuwa wanamdai hiki na kile na hadi mwisho aligonga mwamba.


Nikuulize swali mwanakwetu, ebu fikiria tu filamu hii ya Coming to America wimbo wa To be loved umetumika kwa zaidi ya dakika tatu, je kampuni yenye haki na wimbo huo imelipwa kiasi gani? Kwa hakika ni fedha nyingi.


Kwa mafanikio aliyoyafikia Jackie Wilson anatajwa kuwa ndiye mwanamuziki bora wa milenia huku wengine wanaomsogelea ni Elvis Presley na Michael Jacksoni hii ni kulingana na ubora wa nyimbo zake.


Kwa leo namaliza kwa kusema kuwa, Tanzania tunafanya utekekeleza wa utoaji wa mirabaha ya kazi za sanaa, hili ni jambo jema, lakini tuna wajibu wa kuwaongoza wasanii wetu kuwa makini na mikataba kadhaa wanayoingia na makampuni ambayo yanatayarisha filamu, muziki, na kazi zingine za sanaa. Isijekuwa wasanii Tanzania kivuli cha maisha ya Jackie Wilson.


Msanii anaweza kuwa na kazi nzuri sana lakini sehemu kubwa ya malipo hayo yakazinufaisha kampuni zilizoshirikiana naye kutayarisha kazi hiyo kwa mikataba ya ujanja ujanja.


Simulizi ya Jackie Wilson si kwamba hakukuwa na mikataba na mirabaha, ilikuwapo mwanakwetu, lakini aliambulia patupu.


makwadeladius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI